MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJALI'.

Neno *ajali* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino [Ngeli: i-/-zi]*  yenye maana zifuatazo:

1. Tukio la ghafla lenye madhara au maafa kwa mtu, watu au mali.

2. Tukio la kifo.
*Methali* : *Ajali haina kinga*: Binadamu hana uwezo wa kuzuia maafa.

3. Jambo linalotokana na kudra za Mwenyeezi Mungu; *majaaliwa* .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajali*( *soma: ajalun/ajalan/ajalin اجل )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Muda maalumu. *Likulli Shay-in Ajaluhu لكل شيء أجله* Kila kitu kina muda wake.

2. Wakati maalumu wa kuisha kitu; *kifo* :  *Jaa-a ajaluhu جاء أجله* Kimefika kifo chake.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *ajalun/ajalan/ajalin اجل* llilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajali*  maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu hazikubadilika bali Waswahili wakaliongezea maana ya tukio la ghafla lenye madhara au maafa kwa mtu, watu au mali na ile maana ya jambo linalotokana na kudra za Mwenyeezi Mungu; majaaliwa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*