08-31-2021, 08:13 AM
MASWALI NA MAJIBU -3: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Andika kisawe cha kila neno.
Neno Kisawe
UMOJA WINGI
Mfano: Ng’ombe, mbuzi, kondoo – wanyama
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
MAJIBU
SEHEMU A: Andika kisawe cha kila neno.
Neno Kisawe
- Kifungua mimba ……………….
- Mvulana ……………….
- Fedha ……………….
- Ndovu ……………….
- Kenda ……………….
UMOJA WINGI
- …………….. Mawe
- Sanduku ……………
- ……………… Kwato
- Gulio …………….
- Haraka haraka ………………………….
- ………………………..mauti nyuma
- Haba na haba ………………………..
- Usiache mbachao………………………
- Ndani ya pochi mama aliweka fedha na funguo…………………….(yake, wake,zake)
- Bakari na Mwasiti walipewa ……………….kali(adhabu, adabu, azabu)
- Kuna msemo usemao “siku za mwizi ni ……………(kumi, nyingi, arobaini)
Mfano: Ng’ombe, mbuzi, kondoo – wanyama
- Ugali, wali, ndizi ……………..
- Chungwa, papai, nanasi…………
- Mende, kunguni, chawa……………
- Papa, kambale, perege…………….
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Sisi tunaishi katika kijiji cha Mwambani kandokando ya bahari ya Hindi. Siku moja mjomba wangu alishikwa na homa kali. Alimeza kidonge kwa muda wa siku mbili lakini hakupata nafuu. Siku ya tatu baba na wazee wengine walimpeleka kwenye kituo cha afya.
Kituo cha afya kipo kilometa tano kutoka nyumbani kwetu. Mgonjwa alipelekwa kwa baiskeli. Alipofika kituoni alionana na daktari. Baada ya uchunguzi wa kutosha mjomba aligundulika kuwa na malaria. Daktari alimpeleka wodini na kumlaza kwene kitanda maalumu chenye magurudumu. Mgonjwa alianza kuhudumiwa na wauguzi kwa kupewa dawa na baada ya siku saba tu mjomba Maganga akapona.
MASWALI- Homa kali iliyomshika mjomba Maganga ilitokana na……………
- Mara baada ya mgonjwa kuzidiwa na kufikishwa kituo cha afya jambo gani lilifanyika?
- Mjomba Maganga alipona baada ya muda gani tangu kulazwa kituo cha afya?
- Inatubidi tufanye nini tunaposhikwa na malaria?
- Tunaweza kuepuka malaria kwa kufanyaje?
MAJIBU
- Mwanambee
- mvuli
- tembo
- pesa/hela
- tisa
- jiwe
- masanduku
- ukwato
- magulio
- haina baraka
- tamaa mbele
- hujaza kibaba
- kwa mswala upitao
- zake
- adhabu
- arobaini
- vyakula
- matunda
- wadudu
- samaki
- C
- D
- A
- C
- B
Mwl Maeda