MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI - MASWALI NA MAJIBU -3: DARASA LA 3 & 4

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: MASWALI NA MAJIBU -3: DARASA LA 3 & 4
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
MASWALI NA MAJIBU -3: DARASA LA 3 & 4
SEHEMU A: Andika kisawe cha kila neno.
Neno                                                 Kisawe
  1. Kifungua mimba                         ……………….
  2. Mvulana                                       ……………….
  3. Fedha                                            ……………….
  4. Ndovu                                            ……………….
  5. Kenda                                            ……………….
SEHEMU B: Andika umoja au wingi wa maneno yafuatayo.
         UMOJA                                     WINGI
  1. ……………..                                    Mawe
  2. Sanduku                                       ……………
  3. ………………                                    Kwato
  4. Gulio                                               …………….
SEHEMU C: Kamilisha methali zifuatazo
  1. Haraka haraka ………………………….
  2. ………………………..mauti nyuma
  3. Haba na haba ………………………..
  4. Usiache mbachao………………………
SEHEMU D: Chagua neno sahihi katika mabano ili kukamilisha sentensi zifuatazo:
  1. Ndani ya pochi mama aliweka fedha na funguo…………………….(yake, wake,zake)
  2. Bakari na Mwasiti walipewa ……………….kali(adhabu, adabu, azabu)
  3. Kuna msemo usemao “siku za mwizi ni ……………(kumi, nyingi, arobaini)
SEHEMU E: Andika neno moja lenye maana ya maneno yaliyotolewa.
Mfano: Ng’ombe, mbuzi, kondoo – wanyama
  1. Ugali, wali, ndizi ……………..
  2. Chungwa, papai, nanasi…………
  3. Mende, kunguni, chawa……………
  4. Papa, kambale, perege…………….
SEHEMU F: UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Sisi tunaishi katika kijiji cha Mwambani kandokando ya bahari ya Hindi. Siku moja mjomba wangu alishikwa na homa kali. Alimeza kidonge kwa muda wa siku mbili lakini hakupata nafuu. Siku ya tatu baba na wazee wengine walimpeleka kwenye kituo cha afya.
Kituo cha afya kipo kilometa tano kutoka nyumbani kwetu. Mgonjwa alipelekwa kwa baiskeli. Alipofika kituoni alionana na daktari. Baada ya uchunguzi wa kutosha mjomba aligundulika kuwa na malaria. Daktari alimpeleka wodini na kumlaza kwene kitanda maalumu chenye magurudumu. Mgonjwa alianza kuhudumiwa na wauguzi kwa kupewa dawa na baada ya siku saba tu mjomba Maganga akapona.
MASWALI
  1. Homa kali iliyomshika mjomba Maganga ilitokana na……………
(a) kulogwa (b) kuishi kandokando ya baharo © malaria (d) kumeza vidonge bila kupimwa
  1. Mara baada ya mgonjwa kuzidiwa na kufikishwa kituo cha afya jambo gani lilifanyika?
(a) daktari alimpa dawa (b) alilazwa wodini © kuhudumiwa na wauguzi (d) alifanyiwa uchunguzi
  1. Mjomba Maganga alipona baada ya muda gani tangu kulazwa kituo cha afya?
(a) juma moja (b) siku mbili © siku tano ( muda mfupi)
  1. Inatubidi tufanye nini tunaposhikwa na malaria?
(a) tumeze vidonge (b) twende kwa waganga wa kienyeji © twende hospitali kwa wauguzi na matabibu (d) tusitumie dawa
  1. Tunaweza kuepuka malaria kwa kufanyaje?
(a) kufunga milango (b) kusafisha mazingira yetu na utumiaji vyandarua © kumeza dawa mara kwa mara (d) kulala madirisha wazi
MAJIBU
  1. Mwanambee
  2. mvuli
  3. tembo
  4. pesa/hela
  5. tisa
  6. jiwe
  7. masanduku
  8. ukwato
  9. magulio
  10. haina baraka
  11. tamaa mbele
  12. hujaza kibaba
  13. kwa mswala upitao
  14. zake
  15. adhabu
  16. arobaini
  17. vyakula
  18. matunda
  19. wadudu
  20. samaki
  21. C
  22. D
  23. A
  24. C
  25. B