08-23-2021, 07:14 AM
- Huwa na matumizi makubwa ya utendaji na taharuki
- hutumia mtindo rahisi na lugha rahisi
- dhamira zake hupendwa na watu wengi, hasa vijana
- wahusika wakuu hukwezwa sana kimatendo na sifa zao
- hakuna mpangilio mzuri wa visa na matukio
- hutumia mwendelezo wa wahusika yaani huwa na sifa ya kutumia wahusika wale wale katika mfululizo wa vitabu kadhaa vinavyotolewa na mwandishi.
- huiga mawazo na matendo kutoka fasihi pendwa za nchi zilizoendelea
- huenzi jinsi ya kike kama chombo cha anasa na uhalifu
- mandhari huundwa kwa namna ya kipekee sana
Mwl Maeda