MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: DUNIA MWENDO WA NGISI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: DUNIA MWENDO WA NGISI
#1
DUNIA MWENDO WA NGISI

Nisikilize Kidawa, ewe mwanangu mpendwa
Neno langu nakugawa, kwako liwe la kupandwa
Mwana nikuweke sawa, kesho usijekupindwa
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa.

Kidawa wangu sikia, neno langu ulishike
Babayo nakuambia, nataka uhamasike
Ungali waibukia, sitaki uhasirike
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Tulikulea kwa dhiki, mamiyo kesha kwambia
Mengi hayahesabiki, ambayo tumepitiya
Ila kunena mithaki, yote tumevumilia
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Ungali mkangaichi, maoziyo yana kiwi
Ila hauchi hauchi, kesho yatapata kawi
Daima mficha uchi, uzazini huwa hawi
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Macho utapofumbua, uitazame dunia
Mtima utachanua, uhamu kuchapukia
Mwanangu hili tambua, babayo nashadidia
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Ina vingi vipendezi, vya hadhi na shani yake
Isoisha uchombezi, hutaki hadi utake
Mwana nakupa hirizi, ujikingie makeke
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Dunia tambara bovu, ukivuta utachana
Itakutia makovu, ukichezeya ujana
Ufumbate utulivu, kuepuka kuzozana
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Dunia nzito tambua, endapo huna akili
Yaweza kukuumbua, nakukutia thakili
Leo ninakuzindua, tafakari kulihali
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Dunia ni mduwara, huzunguka kama pia
Kwa idhini na kudura,hujirudia
Usitende kwa hasira, keshoye ukajutia
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Dunia ni mapishano, Leo mbele kesho nyuma
Kuishi ni mapambano, kusotaka uadhama
Kushinda kwenye pigano, mtegemee Karima
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Dunia ni maabara, jaribu hili na lile
Yatende kwa tahadhara, uepuke mizingile
Ujitoapo kafara, dunia ni ile ile
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Dunia ni darubini, kwayo mwana jiakisi
Uishi kwa kubaini, na kuheshimu mapisi
Wenzako usiwahini, kwa tendo au kwa tusi
Dunia mwendo wa ngisi, isikuteke Kidawa

Adamu Djibril
Jibril Adam Abu sanaya
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)