MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MISIMU / SIMO

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MISIMU / SIMO
#1
MISIMU / SIMO
Misimu ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. misimu inayodumu huweza kuingia katika methali, nahau au misemo ya lugha ya jamii hiyo.
CHANZO CHA MISIMU
  • Misimu huzuka kutoka na na mabadiliko ya kihistoria yanayokumba jamii katika nyakati mbalimbali.
  • Misimu mingine huzuka kutokana na hali ya utani miongonim mwa watu mbalimbali.
  • Mara nyingi misimu ya aina hii hubeba kebehi, dhihaka, kejeli, mabezo, dharau au kusifu kusiko kwa kawaida.
SIFA ZA MISIMU
  • Misimu huzuka na kutoweka.
  • Misimu ni lugha isiyo rasmi.
  • Misimu ni lugha ya mafumbo.
  • Misimu ina chuku nyingi.
  • Misimu ina maana nyingi.
  • Misimu hupendwa sana na wengi.
  • Misimu ina mvuto na kwa sababu hii hupendwa na watu wengi.
  • Misimu huhifadhi historia ya ya jamii.
SABABU ZA KUTUMIA MISIMU
  • Kutaka mazungumzo yawe siri.
  • Kudhania matumizi ya misimu ndio ujuzi wa lugha.
  • Kufanya mambo mazito naya maana kuwa mepesi naya kawaida.
NJIA ZITUMIKAZO KUUNDA MISIMU
  • Njia ya kufupisha maneno (Kufupisha maneno mfano Kompyuta –komp)
  • Njia ya kutohoa kutoka lugha za kigeni. (Kutotoa maneno ya kigeni mfano father- fadhee)
  • Njia ya kutumia sitiari (Kutumia sitiari au jazanda mfano-Golikipa –Nyani, Mtu mlafi-fisi)
  • Njia ya kutumia tanakali (Kutumia tanakalimfano; Bunduki – mtutu)
  • Njia ya kubadili maana ya msingi
AINA ZA MISIMU
  1. Misimu ya pekee
Huelezea uhusiano uliopo kati ya kikundi kimoja kutoka kwenye utamaduni mmoja. Misimu hii inapatikana sehemu fulani ambapo wanaishi watu wa aina moja, mfano kazini. Misimu hii inaitwa ya kipekee kwa sababu hujulikana sehemu ilipozukia tu, na sio nje ya eneo hilo.
Kwa mfano misimu ya kipekee inaweza kutumiwa na: –
  • Wafanyakazi katika ofisi moja
  • wanafunzi katika shule moja
  • wanamichezo wa sehemu fulani.
  1. Misimu ya kitarafa
Misimu ya kitarafa huchukua eneo kubwa/pana kidogo kimatumizi inaweza kutumika hata kwenye tarafa, wilaya, mkoa au kanda. Ueneaji wa misimu hii hutegemea hali au tabia ya muingiliano wa watu katika shughuli za maisha ya kila siku, kama- biashara na michezo, mara kadhaa misimu ya kitarafa hutokana na:[Image: 4avBUgrVUAfbUJ-mrrjuF665ZrO8ZwykaxuDujoD...cIt6H4S6Cw]
  • Vitu vilivyo katika eneo fulani
  • Lugha itumikayo katika eneo fulani
  • Uzoefu wa mazingira au uwezo wa lugha ya msanii.
  1. Misimu zagao
Misimu zagao huenea nchi nzima pengine hata kuvuka mipaka ya nchi. Misimu zagao hutumika katika mikoa yote ya nchi na pia hutumika katika vyombo vya habari kama vile magazeti, hutumika pia katika vitabu na vipindi vya redio na television.
Mfano wa misimu zagao ni: –  neno (kabwela), (wakereketwa), (buzi), (bwege) n.k

MATUMIZI /DHIMA ZA MISIMU
  • Kukuza Lugha
  • kupamba lugha
  • Kufanya mawasiliano yawe mafupi na yanayoeleweka kwa haraka
  • Kuficha lugha ya matusi
  • Kuwaunganisha watu wa makundi (matabaka) mbalimbali
  • Kuhifadhi historia ya jamii.
  • Kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji
  • Kufurahisha na kuchekesha
  • Kukosoa na kuiasa jamii
  • Misimu huleta msamiati wenye matusi
  • Misimu hupunguza hadhira
MATATIZO YA MISIMU
  • Misimu huharibu lugha kwa sababu siyo lugha sanifu
  • Misimu baadhi ya wakati huleta msamiati yenye matusi
  • Misimu ni lugha ya mafumbo na hufahamika na kikundi kidogo kinachotumia misimu hiyo.
  • Misimu imetiwa chumvi nyingi kwa hivyo haiaminiki katika jamii
  • Misimu huzuka na kutoweka
  • Misimu ina maana nyingi
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)