MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

Nyenzo­rejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Nyenzo­rejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi
#1
Nyenzo­rejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi
[Image: note.png] Nyenzo Rejea ya mwalimu kwa upangaji au kurekebisha kwa ajili ya kutumia na wanafunzi
Mfano wa wimbo wa Kiswahili
Wimbo wa kubembelezea mtoto wa ‘Kua’, unahusu mzazi anayekazania kumwambia mtoto wake mdogo akue. Zingatia mdafao wa marudio ya herufi na sauti zilezile.
Unaimbwa hivi:
Quote:‘Kua mwanangu, kua. Kua ili nikupe mawaidha ili kwamba niweze kukupa kundi la ng’ombe na mbuzi, ili upate maziwa. Kua mwanangu, kua. Kua ili uwe mkubwa. Kua upesi kama mgomba kwa sababu mnazi unachelewa. ‘Kua mwanangu, kua.
Katika unaweza kuusikia wimbo huu.
Vyanzo vya asili: [BBC Radio 3 On Your Stree], Website
Shairi la Kiswahili lililotafsiriwa kutoka lugha ya Kiiingereza ambalo linafurahisha likighanwa harakaharaka
Siagi ya Manjano na Mary Ann Hoberman
Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi
Ipakaze kwa wingi
Iseme kwa haraka
Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi
Ipakaze kwa wingi sana
Iseme kwa haraka sana
Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi
Sasa irudie
Ukiwa unaila
Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi
Usiongee mdomo ukiwa umejaa!
Shairi la vitendo
Mimi ni chombo kidogo cha sukari, kifupi na imara
Huu ni mpini wangu, huu ni mdomo wangu
Ninapopata joto
Hapo ninapayuka
Nipindue
Nimwage.
Wimbo wa mnyama dunia – wimbo kutoka Kongo
Angalizo: Wimbo huu unahusu harakati na sauti za kiitikio zinawakilisha harakati za viumbe.
MSIMULIAJI: Samaki huenda
KIITIKIO: Hip!
MSIMULIAJI: Ndege huenda
KIITIKIO: Viss! MSIMULIAJI: Nyani huenda KIITIKIO: Nyan!
SAMAKI: Ninaanzia kushoto,
Ninageuka kulia.
Mimi ni samaki
Anayeponyoka majini,
Anayeteleza,
Anayenengua,
Anayechupa!
 
MSIMULIAJI: Kila kitu kinaishi,
Kila kitu hucheza dansi,
Kila ktu huimba.
KIITIKIO: Hip!
Viss!
Nyan!
 
NDEGE: Ndege huruka mbali,
Huruka, huruka, huruka,
Huenda, hurudi, hupita,
Hupanda, huelea, hutua.
Mimi ni ndege!
 
MSIMULIAJI: Kila kitu huishi,
Kila kitu hucheza dansi,
Kila kitu huimba.
KIITIKIO: Hip!
Viss!
Nyan!
 
NYANI: Nyani! Kutoka tawi
hadi tawi
Hukimbia, huchupa, huruka,
Akiwa na mkewe na mtoto,
Mdomo ukiwa umejaa chakula, mkia hewani,
Huyu ni nyani!
Huyu ni nyani!
 
MSIMULIAJI: Kila kitu huishi,
Kila kitu hucheza dansi,
Kila ktu huimba.
KIITIKIO: Hip!
Viss!
Nyan!
Vyanzo vya asili: [Siagi ya manjano – Shairi/wimbo wa jadi; Kiingereza Kipya cha Mafanikio, Darasa la 6, Kitabu cha Kusoma], [Oxford University Press]
[ Wimbo wa mnyama dunia – Wimbo wa jadi kutoka Kongo], [Ushairi wa Kiafrika kwa Shule, Longman]
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)