Nyenzorejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Stashahada/Cheti (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=21) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=25) +----- Thread: Nyenzorejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi (/showthread.php?tid=701) |
Nyenzorejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi - MwlMaeda - 08-01-2021 Nyenzorejea ya 2: Mifano ya nyimbo na mashairi Nyenzo Rejea ya mwalimu kwa upangaji au kurekebisha kwa ajili ya kutumia na wanafunzi
Mfano wa wimbo wa Kiswahili
Wimbo wa kubembelezea mtoto wa ‘Kua’, unahusu mzazi anayekazania kumwambia mtoto wake mdogo akue. Zingatia mdafao wa marudio ya herufi na sauti zilezile. Unaimbwa hivi: Quote:‘Kua mwanangu, kua. Kua ili nikupe mawaidha ili kwamba niweze kukupa kundi la ng’ombe na mbuzi, ili upate maziwa. Kua mwanangu, kua. Kua ili uwe mkubwa. Kua upesi kama mgomba kwa sababu mnazi unachelewa. ‘Kua mwanangu, kua.Vyanzo vya asili: [BBC Radio 3 On Your Stree], Website Shairi la Kiswahili lililotafsiriwa kutoka lugha ya Kiiingereza ambalo linafurahisha likighanwa harakaharaka
Wimbo wa mnyama dunia – wimbo kutoka KongoSiagi ya Manjano na Mary Ann Hoberman Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi Ipakaze kwa wingi Iseme kwa haraka Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi Ipakaze kwa wingi sana Iseme kwa haraka sana Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi Sasa irudie Ukiwa unaila Siagi ya manjano jeli ya zambarau jemu nyekundu mkate mweusi Usiongee mdomo ukiwa umejaa! Shairi la vitendo Mimi ni chombo kidogo cha sukari, kifupi na imara Huu ni mpini wangu, huu ni mdomo wangu Ninapopata joto Hapo ninapayuka Nipindue Nimwage. Angalizo: Wimbo huu unahusu harakati na sauti za kiitikio zinawakilisha harakati za viumbe. MSIMULIAJI: Samaki huenda KIITIKIO: Hip! MSIMULIAJI: Ndege huenda KIITIKIO: Viss! MSIMULIAJI: Nyani huenda KIITIKIO: Nyan! SAMAKI: Ninaanzia kushoto, Ninageuka kulia. Mimi ni samaki Anayeponyoka majini, Anayeteleza, Anayenengua, Anayechupa! MSIMULIAJI: Kila kitu kinaishi, Kila kitu hucheza dansi, Kila ktu huimba. KIITIKIO: Hip! Viss! Nyan! NDEGE: Ndege huruka mbali, Huruka, huruka, huruka, Huenda, hurudi, hupita, Hupanda, huelea, hutua. Mimi ni ndege! MSIMULIAJI: Kila kitu huishi, Kila kitu hucheza dansi, Kila kitu huimba. KIITIKIO: Hip! Viss! Nyan! NYANI: Nyani! Kutoka tawi hadi tawi Hukimbia, huchupa, huruka, Akiwa na mkewe na mtoto, Mdomo ukiwa umejaa chakula, mkia hewani, Huyu ni nyani! Huyu ni nyani! MSIMULIAJI: Kila kitu huishi, Kila kitu hucheza dansi, Kila ktu huimba. KIITIKIO: Hip! Viss! Nyan! Vyanzo vya asili: [Siagi ya manjano – Shairi/wimbo wa jadi; Kiingereza Kipya cha Mafanikio, Darasa la 6, Kitabu cha Kusoma], [Oxford University Press] [ Wimbo wa mnyama dunia – Wimbo wa jadi kutoka Kongo], [Ushairi wa Kiafrika kwa Shule, Longman] |