Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu
bikariolezi
kichopeko
kidira
kisuwembe
maleti mpira
mwega feleji
ngoeko
panchi gezamguu
panchi mzunguko
Bb
bikariolezi ji wing dividers: bikari itumiwayo na mafundi, k.m., seremala, fundi viatu, n.k., kutengeneza violezo.
bikariolezi
Kk
kichopeko ji shoe horn: kifaa maalum kinachosaidia kuingiza mguu kwenye kiatu wakati wa kukivaa.
kichopeko
kidira ji cutting nipper: Kifaa cha kukata na kung’oa misumari.
kidira
kisuwembe ji rampat edger: kifaa mfano wa wembe ambacho hutumiwa kwa ajili ya kukatia ngozi.
kisuwembe
Mm
maleti mpira ji rubber mallet: nyundo kubwa ambayo kichwa chake ni mpira.
maleti mpira
mwega feleji ji iron rest: pande la chuma ambalo juu yake huwekwa kiatu wakati wa kugongwa misumari.
mwega feleji
Nn
ngoeko ji hook: kifaa cha kukamatia au kutolea ubaowayo kwenye kiatu.
ngoeko
Pp
panchi gezamguu ji wooden hole punch: ubao uliochongwa kulingana na nambari tofauti za miguu ya watu.
panchi gezamguu
panchi mzunguko ji revolving punch: chuma chenye meno ya kutobolea matundu kwenye ngozi.
panchi mzunguko
Rr
riveti ji eyelet: metali zenye vitobo zinazowekwa kwenye vitundu katika viatu, nguo, n.k.
riveti
Mwl Maeda