Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Kamusi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=70) +--- Thread: Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu (/showthread.php?tid=352) |
Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu - MwlMaeda - 06-29-2021 Vidahizo vya Fani ya Ufundi Viatu Bb
bikariolezi ji wing dividers: bikari itumiwayo na mafundi, k.m., seremala, fundi viatu, n.k., kutengeneza violezo.
bikariolezi Kk
kichopeko ji shoe horn: kifaa maalum kinachosaidia kuingiza mguu kwenye kiatu wakati wa kukivaa.
kichopeko kidira ji cutting nipper: Kifaa cha kukata na kung’oa misumari.
kidira kisuwembe ji rampat edger: kifaa mfano wa wembe ambacho hutumiwa kwa ajili ya kukatia ngozi.
kisuwembe Mm
maleti mpira ji rubber mallet: nyundo kubwa ambayo kichwa chake ni mpira.
maleti mpira mwega feleji ji iron rest: pande la chuma ambalo juu yake huwekwa kiatu wakati wa kugongwa misumari.
mwega feleji Nn
ngoeko ji hook: kifaa cha kukamatia au kutolea ubaowayo kwenye kiatu.
ngoeko Pp
panchi gezamguu ji wooden hole punch: ubao uliochongwa kulingana na nambari tofauti za miguu ya watu.
panchi gezamguu panchi mzunguko ji revolving punch: chuma chenye meno ya kutobolea matundu kwenye ngozi.
panchi mzunguko Rr
riveti ji eyelet: metali zenye vitobo zinazowekwa kwenye vitundu katika viatu, nguo, n.k.
riveti
|