MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO "BINAMU''

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO "BINAMU''
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO "BINAMU''

Neno *binamu* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/wa-*] yenye maana ya mtoto wa kike au wa kiume wa shangazi au mjomba.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *binamu* limechukuliwa kutoka maneno mawili ya Kiarabu *bun (ibnu) بن/ابن na ammi (soma: ammun/amman/ammin عم).* 

Neno *ibnu/bnu بن/ابن* lina maana ya mtoto wa kiume. Unaposema: Khamis bun Said, maana yake ni: Khamis mtoto wa kiume wa Said.

Watu wa Mauritania badala ya neno *bun بن* wao hutumia neno *walad ولد* neno la Kiarabu lenye maana ya mtoto wa kiume. Yaani: *Khamis bun Said* Wa-Mauritania husema: *Khamis Walad Said.*

Na neno *ammun عم* lina maana ya ndugu wa kiume wa baba.

Neno hilo pia lina maana ya kundi la watu wengi, majani (nyasi) na mtende mrefu.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno ya Kiarabu *'ibnu ammi  ابن عم* yenye maana ya mtoto wa kiume wa ndugu wa kiume wa baba yalipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *binamu* yalichukua maana mpya ya mtoto wa kike au wa kiume wa shangazi au mjomba.

*TANBIHI:*
Katika lugha ya Kiarabu neno *ibnu* hutumika katika lugha ya mafumbo kama vile:
1. *Ibnus Swulbi ابن الصلب* (mtoto wa uti wa mgongo) kwa maana ya mtoto halisi/mtoto halali kisheria.
2. *Ibnu Amsi/Albaariha ابن امس/البارحة* (mtoto wa jana) kwa maana ya mtu asiye na tajriba ya maisha.
3. *Ibnu Batwinihi ابن بطنه* (mtoto wa tumbo lake) kwa maana ya mchumia tumbo.
4. *Ibnu Jalaa ابن جلا* (mtoto wa wanja)  kwa maana ya mtu mashuhuri maarufu.
5. *Ibnul Balad ابن البلد* (mtoto wa mjini) kwa maana ya mtu anayeishi katika mji aliozaliwa na kukulia.
6. *Ibnul Halaali ابن الحلال* (mtoto wa halali) kwa maana ya mtoto aliyezaliwa ndani ya ndoa ya kisheria.

Katika lugha ya Kiarabu, shangazi huitwa *ammat عمة* na mtoto wa shangazi huitwa *ibnu ammat ابن عمة* na mjomba huitwa *khaalun خال* na mtoto wa mjomba huitwa *ibnu Khaalin ابن خال.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)