MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'PUNGUANI, HAYAWANI ' NA 'MAJNUNI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO 'PUNGUANI, HAYAWANI ' NA 'MAJNUNI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'PUNGUANI, HAYAWANI ' NA 'MAJNUNI'

Maneno *punguani, hayawani na majnuni* yanatumika kwa maana ya mtu ambaye akili zake zina hitilafu; mwendawazimu, chizi, kichaa, mwehu.

Neno *punguani* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [ *Ngeli: a-/wa-]* yenye maana ya mtu ambaye akili zake zina hitilafu; mwendawazimu, chizi, majnuni.

Neno *punguani* pia ni kivumishi chenye maana ya '-enye akili zisizotimia; pungufu wa akili.

Neno hili *punguani* etimolojia yake ni Kibantu na linatokana na kitenzi si elekezi *pungua*  ambacho moja ya maana zake ni *kuwa na hitilafu; kutotimia.*

Neno *hayawani* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [ *Ngeli: a-/wa-, wingi: mahayawani]* yenye maana zifuatazo:

1. Mnyama.

2. Mtu anayefananishwa na mnyama aghalabu asiye na adabu.

3. Mtu asiye na nidhamu.

4. Mwendawazimu, mwehu, kichaa, chizi.

5. Shetani.

Katika lugha ya Kiarabu, neno  *hayawani* limetokana na neno la Kiarabu *hayawaanun* (soma: *hayawaanun/hayawaanan/hayawaanin  حيوان* ) lenye maana zifuatazo:

1. Kiumbe hai kinachojipambanua kwa kuwa na uhai, hisi na harakati; kila kilicho hai chenye kinachosema ( mwanadamu ambaye huitwa *hayawaanun naatwiqun حيوان ناطق* mnyama mwenye kusema) na mnyama asiyesema (baki ya wanyama wengineo).

2- Mnyama mwenye sifa ya mmea *hayawaanun nabaatiy* *حيوان نباتي* mnyama anayefanana na umbo la mmea kama *sifongo*.

3- Mnyama wa medula *hayawaanun nakhaaiyun حيوان نخاعي*  mnyama wa uti wa mgongo, mwenye uti wa mgongo lakini hana ubongo.

4- Mbegu ya uzazi: manii.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *hayawaanun/hayawaanan/hayawaanin حيوان*) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *hayawani*  lilichukua katika lugha ya asili - Kiarabu maana za mnyama na mwendawazimu, kulipa maana mpya ya mtu asiye na aibu/nidhamu na kuacha maana zingine.

Neno *majinuni* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [ *Ngeli: a-/wa-]*  yenye maana ya mtu asiye na akili.

Neno hili *majinuni* linatokana na neno la Kiarabu *majnuun* (soma: *majnuunun/majnuunan/majnuunin محنون* ) lenye maana ya mtu asiye na akili.

Kinachodhihiri ni kuwa maana za maneno ya Kiarabu *hayawanun* na *majnuunun* yalipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa hayawani na majinuni hayakubadili maana ya mtu asiye na akili.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)