MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA'

Neno badana katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-] yenye maana ya wanyama kama vile ng'ombe, kondoo, ngamia wanaochinjwa kuwa sadaka siku ya ibada ya Hija.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili badana limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu  'badanah( soma: badanatun/badanatan/badanatin بدنة ) ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Ngamia au ng'ombe anayepelekwa Makkah kwa ajili ya kuchinjwa wakati wa kutekeleza ibada ya Hijja.

2. Ng'ombe au ngamia aliyenenepeshwa.

3. Nguo ivaliwayo na wanawake aghalabu hupasuliwa bila ya kuwekwa mikono.

Kinachodhihiri ni kuwa neno 'badanatun بدنة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno badana lilichukua kutoka Kiarabu maana ya wanyama howa wanaopelekwa Makkah kuchinjwa wakati wa ibada ya Hija na kuacha maana ya nguo ya kike inayopasuliwa bila ya kuwekwa mikono.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)