ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA' (/showthread.php?tid=2601) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA' - MwlMaeda - 06-16-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'BADANA' Neno badana katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/wa-] yenye maana ya wanyama kama vile ng'ombe, kondoo, ngamia wanaochinjwa kuwa sadaka siku ya ibada ya Hija. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili badana limechukuliwa kutoka neno la Kiarabu 'badanah( soma: badanatun/badanatan/badanatin بدنة ) ambalo ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo: 1. Ngamia au ng'ombe anayepelekwa Makkah kwa ajili ya kuchinjwa wakati wa kutekeleza ibada ya Hijja. 2. Ng'ombe au ngamia aliyenenepeshwa. 3. Nguo ivaliwayo na wanawake aghalabu hupasuliwa bila ya kuwekwa mikono. Kinachodhihiri ni kuwa neno 'badanatun بدنة lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno badana lilichukua kutoka Kiarabu maana ya wanyama howa wanaopelekwa Makkah kuchinjwa wakati wa ibada ya Hija na kuacha maana ya nguo ya kike inayopasuliwa bila ya kuwekwa mikono. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |