MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI'

Neno *arubasitini*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Makumi sita na mamoja manne.

2. Mchezo wa karata ambapo karata inayotawala ndiyo huongoza mchezo na mshindi hupatikana kwa kupata idadi ya 60 kwenda juu.

Neno *arubasitini* limechukuliwa kutoka maneno mawili ya Kiarabu *arbau* na *sittuuna* ( *soma: arbau wa sittuuna/arbaa wa sittiina  اربع وستون/اربع وستين )*  yenye maana ya makumi sita na mamoja manne; sitini na nne (64).

Kinachodhihiri ni kuwa nomino ya Kiarabu  *arbau wa sittuuna اربع وستون* ilipoingia  katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arubasitini* halikubadili maana yake inayohusu idadi katika lugha asili - Kiarabu bali lilibeba maana mpya ya mchezo wa karata ambapo karata inayotawala ndiyo huongoza mchezo na mshindi hupatikana kwa kupata idadi ya 60 kwenda juu.

*TANBIHI:*
1. Mchezo wa karata - *arubasitini* - ni mashuhuri sana pwani ya Afrika Mashariki na kule Ujerumani kuna mchezo wa karata wa 66 (Kijerumani: *Sechsundsechzig*), ambao wakati mwengine hujulikana kama *Paderbörnern.*

2. Kamusi za Kiswahili zimesajili maneno mengine yanayohusu idadi kama vile arubaishirini (24), arubamia (400), arubatashara (14), maneno ambayo hutumika zaidi katika mashairi na tenzi si katika mawasiliano ya kawaida.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)