ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI' (/showthread.php?tid=2580) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI' - MwlMaeda - 05-25-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ARUBASITINI' Neno *arubasitini* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Makumi sita na mamoja manne. 2. Mchezo wa karata ambapo karata inayotawala ndiyo huongoza mchezo na mshindi hupatikana kwa kupata idadi ya 60 kwenda juu. Neno *arubasitini* limechukuliwa kutoka maneno mawili ya Kiarabu *arbau* na *sittuuna* ( *soma: arbau wa sittuuna/arbaa wa sittiina اربع وستون/اربع وستين )* yenye maana ya makumi sita na mamoja manne; sitini na nne (64). Kinachodhihiri ni kuwa nomino ya Kiarabu *arbau wa sittuuna اربع وستون* ilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *arubasitini* halikubadili maana yake inayohusu idadi katika lugha asili - Kiarabu bali lilibeba maana mpya ya mchezo wa karata ambapo karata inayotawala ndiyo huongoza mchezo na mshindi hupatikana kwa kupata idadi ya 60 kwenda juu. *TANBIHI:* 1. Mchezo wa karata - *arubasitini* - ni mashuhuri sana pwani ya Afrika Mashariki na kule Ujerumani kuna mchezo wa karata wa 66 (Kijerumani: *Sechsundsechzig*), ambao wakati mwengine hujulikana kama *Paderbörnern.* 2. Kamusi za Kiswahili zimesajili maneno mengine yanayohusu idadi kama vile arubaishirini (24), arubamia (400), arubatashara (14), maneno ambayo hutumika zaidi katika mashairi na tenzi si katika mawasiliano ya kawaida. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |