MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI'

Neno *asherati* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/wa-*] yenye maana ya *mtu mwenye tabia  ya kujamiiana na mtu au watu wasiokuwa na uhusiano wa kindoa.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *asherati* linatokana na nomino ya Kiarabu *ashiirah (soma: ashiiratun/ashiiratan/ashiiratin  عشيرة)*  lenye maana zifuatazo:

1. Rafiki.

2. Jamaa wa karibu.

3. Mke, *haadhihii ashiiratii هذه عشيرتي* huyu ni mke wangu, *haadhaa ashiirii هذا عشيري* huyu ni mume wangu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *ashiirat* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *asherati* lilichukua maana mpya ya  mtu mwenye tabia  ya kujamiiana na mtu au watu wasiokuwa na uhusiano wa kindoa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)