MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI' - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI' - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16)
+--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI' (/showthread.php?tid=2557)

ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI' - MwlMaeda - 05-11-2022

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ASHERATI'

Neno *asherati* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: a-/wa-*] yenye maana ya *mtu mwenye tabia  ya kujamiiana na mtu au watu wasiokuwa na uhusiano wa kindoa.*

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *asherati* linatokana na nomino ya Kiarabu *ashiirah (soma: ashiiratun/ashiiratan/ashiiratin  عشيرة)*  lenye maana zifuatazo:

1. Rafiki.

2. Jamaa wa karibu.

3. Mke, *haadhihii ashiiratii هذه عشيرتي* huyu ni mke wangu, *haadhaa ashiirii هذا عشيري* huyu ni mume wangu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *ashiirat* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *asherati* lilichukua maana mpya ya  mtu mwenye tabia  ya kujamiiana na mtu au watu wasiokuwa na uhusiano wa kindoa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*