MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO ' REHEMA' na 'BARAKA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO ' REHEMA' na 'BARAKA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' REHEMA' na 'BARAKA'

Neno *rehema* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [ *Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Neema, heri au baraka anazopata mtu kutoka kwa Mungu.

2. Huruma; moyo wa huruma.

*Mfano:* Kupona katika ajali ile ni kwa rehema za Mungu tu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *rehema* limetokana na neno la Kiarabu *rahma* (soma: *rahmatun/rahmatan/rahmatin رحمة* ) lenye maana zifuatazo:

1. Heri na neema.

2. Msamaha.

3. Upole na huruma.

4. Moyo wa huruma.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *rahmatun/rahmatan/rahmatin رحمة*) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *rehema*  maana yake katika Kiarabu haikubadilika bali iliongezwa maana mpya ya *baraka*  neno ambalo katika Kiarabu linajitegemea Kisemantiki.

Neno *baraka* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* jumla ya mambo yote mazuri katika maisha ya mtu.

2. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* jina la mtu aghalabu mwanamume lenye maana ya ulinzi na upendeleo wa Mungu kwa mtu katika mambo yote.

Neno hili *baraka* (soma: *barakatun/barakatan/barakatin بركة* ) katika lugha ya  Kiarabu lina maana zifuatazo:

1. Maendeleo, kukua na ustawi.

2. Nyongeza, ziada.

3. Furaha, uchangamfu,  starehe.

4. *Habasoda* ; aina ya mbegu zenye rangi nyeusi kama vile za vitunguu ambazo hutibu maradhi mbalimbali, *habbatul barakah حبة البركة* mbegu za baraka.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *baraka*(soma: *barakatun/barakatan/barakatin بركة*) lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *baraka* lilichukua maana mpya ya *jumla ya mambo yote mazuri katika maisha ya mtu* na pia jina la mtu aghalabu mwanaume lenye maana ya *ulinzi na upendeleo wa Mungu kwa mtu katika mambo yote.*

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)