MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ALASIRI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ALASIRI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ALASIRI'

Neno *alasiri*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo:

1. Kipindi cha siku kati ya saa tisa mchana hadi saa kumi na moja  na  nusu jioni. (Kamusi ya Karne ya 21, imesajili alasiri ni muda baina ya saa nane jioni na saa Kumi na moja jioni.)

2. Kipindi cha Swala ya Waislamu baina ya saa tisa na kumi na mbili jioni.

Katika lugha ya Kiarabu neno *alasiri* linatokana na neno la Kiarabu  *al-aswru (soma: al-aswru/al-aswra/al-aswri العصر)* lenye maana  zifuatazo:

1. Kipindi kinachonasibishwa na mtu fulani, dola fulani na mfano wa hayo. *Aswru Shaikhi Ali Hasan Mwinyi عصر الشيخ  علي حسن مويني* zama za Mzee Ali Hasan Mwinyi.

2. Wakati kivuli cha kitu kinapokuwa mfano wake au zaidi; *wakati wa Swala ya Alasiri.*

Kinachodhihiri ni kuwa neno *al-aswru  العصر*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *alasiri* maana yake ya msingi katika lugha ya asili - Kiarabu inayohusu muda wa Swala ya Alasiri haikubadilika na maana ya jumla ya wakati unaonasibishwa na mtu fulani au dola fulani iliachwa.

*TANBIHI:*
Kutumia saa kubaini wakati wa Swala ya Alasiri si kipimo sahihi na maana hiyo itahusika tu na nchi/maeneo ambayo muda uliyotajwa unaafikiana na muda wa Swala ya Alasiri si kinyume chake.
Kipimo sahihi ni kuwa wakati wa Swala ya Alasiri ni pale kivuli kinapokuwa mfano kitu husika hadi kivuli kinapokuwa mara mbili ya mfano wa kitu husika. Mwisho wa wakati wa Swala ya Alasiri ni kuzama Jua na huo ni mwanzo wa wakati wa Swala ya Magharibi.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)