MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'ADUI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'ADUI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'ADUI'

Neno *adui* katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: a-/wa- wingi: maadui]* mtu, mnyama au kiumbe chochote kinachofanyia kiumbe kingine uovu; mtu aliye dhidi yako, kitu kibaya unachopambana nacho kwa mfano: magonjwa, njaa, chuki, wivu, ujinga na kadhalika.

*Methali* : adui wa mtu ni mtu, adui mpende, adui aangukapo mnyanyue.

2. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mtu unayekabiliana naye katika mchezo; *mshindani* .

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *adui*( *soma: aduwwun/aduwwan/aduwwin عدو)*  ni nomino ya Kiarabu  yenye maana ya mtu aliye dhidi yako; hasimu wako, mgomvi wako.

Waarabu wana msemo: *aduwwun aaqilun khayrun min swadiiqin jaahilin عدو عاقل خير من صديق جاهل* adui mwerevu ni bora kuliko rafiki mjinga.

Katika Qur'aan Tukufu, Sura ya 2 (Surat Al-Baqarah), Aya ya 168 shetani ametangazwa kuwa adui wa mwanadamu. Imeandikwa: *Walaa Tattabiu Khutwuwaatish Shaytwaani Innahuu Lakum Aduwwum Mubiin. ولا تتبعوا خطوات الشيطان إنه لكم عدو مبين* Wala usifuate nyendo za shetani, hakiki yeye ni adui aliye wazi.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *aduwwun/aduwan/aduwwin عدو)* lilipoingia katika Kiswahili  na kutoholewa kuwa neno *adui* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu haikubadilika bali iliongezeka maana ya mtu unayekabiliana naye katika mchezo; *mshindani* .

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)