MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA'

Neno *akiba* katika lugha Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya kitu kilichohifadhiwa/kilichowekwa ili kitumike baadaye. 

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *akiba* linafanana kimatamshi na neno *aaqiibatun عاقبة*  lakini limetoholewa kutoka neno la Kiarabu *haqiibatun حقيبة*.

Neno la Kiarabu *aaqibatun عاقبة*  lina maana zifuatazo:

1. Mwisho wa jambo; *hatima* .

2. Malipo anayolipwa mtu mwishoni mwa jambo.

Na neno la Kiarabu *haqiibatun حقيبة*  lina maana zifuatazo:

1. Chombo cha kuhifadhiwa vitu.

2. Kitu kinabebwa safarini ili kumfaa msafiri njiani au aendako.

3. Tumaini la mtu mwisho wa umri wake; mtoto, kizazi. 

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiswahili *akiba* ingawa linafanana kimatamshi  na neno la Kiarabu *aaqibatun عاقبة* lenye maana ya mwisho wa jambo; hatima na malipo anayolipwa mtu mwishoni mwa jambo, limeazimwa na kutoholewa kutoka neno la Kiarabu *haqiibatun حقيبة* (mkoba) lenye maana ya: chombo cha kuhifadhiwa vitu; mkoba, kitu kinabebwa safarini ili kumfaa msafiri njiani au aendako na tumaini la mtu mwisho wa umri wake; mtoto, kizazi. 

Kupewa neno *akiba* maana iliyopewa katika Kiswahili bila shaka ni kuzingatiwa kutaja mkoba kwa kukusudia kilichobebwa mkobani, yaani *dhikrul  haamili Li-iraadatil Mahmuul Fiihi ذكر الحامل* لإرادة المحمول فيه yaani, badala ya kutajwa kilichobebwa mkobani ili kumfaa mbebaji ukatajwa mkoba wenyewe *akiba (haqiibatun حقيبة*).

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)