ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA' (/showthread.php?tid=2454) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA' - MwlMaeda - 03-13-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AKIBA' Neno *akiba* katika lugha Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya kitu kilichohifadhiwa/kilichowekwa ili kitumike baadaye. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *akiba* linafanana kimatamshi na neno *aaqiibatun عاقبة* lakini limetoholewa kutoka neno la Kiarabu *haqiibatun حقيبة*. Neno la Kiarabu *aaqibatun عاقبة* lina maana zifuatazo: 1. Mwisho wa jambo; *hatima* . 2. Malipo anayolipwa mtu mwishoni mwa jambo. Na neno la Kiarabu *haqiibatun حقيبة* lina maana zifuatazo: 1. Chombo cha kuhifadhiwa vitu. 2. Kitu kinabebwa safarini ili kumfaa msafiri njiani au aendako. 3. Tumaini la mtu mwisho wa umri wake; mtoto, kizazi. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiswahili *akiba* ingawa linafanana kimatamshi na neno la Kiarabu *aaqibatun عاقبة* lenye maana ya mwisho wa jambo; hatima na malipo anayolipwa mtu mwishoni mwa jambo, limeazimwa na kutoholewa kutoka neno la Kiarabu *haqiibatun حقيبة* (mkoba) lenye maana ya: chombo cha kuhifadhiwa vitu; mkoba, kitu kinabebwa safarini ili kumfaa msafiri njiani au aendako na tumaini la mtu mwisho wa umri wake; mtoto, kizazi. Kupewa neno *akiba* maana iliyopewa katika Kiswahili bila shaka ni kuzingatiwa kutaja mkoba kwa kukusudia kilichobebwa mkobani, yaani *dhikrul haamili Li-iraadatil Mahmuul Fiihi ذكر الحامل* لإرادة المحمول فيه yaani, badala ya kutajwa kilichobebwa mkobani ili kumfaa mbebaji ukatajwa mkoba wenyewe *akiba (haqiibatun حقيبة*). *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |