MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'HAYATI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'HAYATI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'HAYATI'

Neno *hayati* katika lugha Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mtu hai anayeombewa rehema za Mwenyeezi Mungu.

2. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mtu aliyekwishafariki dunia.

*Msemo: si hayati si mamati*: si mzima, si marehemu, hali yake ni mbaya sana, taabani, hajijui, hajitambui.

3. *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* uhai, au uzima, 'wakati' au 'enzi' ya kipindi fulani cha mtu aliye hai.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *hayati*( *soma: hayaatun/hayaatan/hayaatin حياة)*  ni nomino ya Kiarabu  yenye maana zifuatazo:

1. Kukua, maendeleo, kubakia.

2. Manufaa.

3. Katika elimu ya Bailojia *ilmul ahyaai علم الأحياء*: jumla ya vinavyoshuhudiwa kwa wanyama na mimea miongoni mwa sifa bainifu zinazowatofautisha  na maada, mfano: kula, kukua, kuzaana na mfano wa hayo.

4. Kipindi kati ya kuzaliwa na kufa; siku na miaka.

5. Kiwango cha maisha.

6. Maisha kwa ujumla, kwa mfano: maisha ya mjini, maisha ya kijijini.

7. Kuendelea kubakia mwanadamu, mnyama na mmea na uzima wake, harakati zake na kukua kwake.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu  *hayaatun/hayaatan/hayaatin حياة)* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *hayati*  lilichukua kutoka lugha yake ya asili - Kiarabu maana ya mtu hai na  kupewa maana mpya ya mtu aliyekwishafariki.

*Tanbihi:*
Maana ya neno *hayati* kuwa mtu aliyekwishafariki, yumkini imetokana na imani ya Kiislamu ya kutekeleza maagizo ya Mwenyeezi Mungu ya kutowaita watu wema waliofariki kwa jina la *wafu (maiti)* kwa kuwa wao ni watu hai wanaopewa riziki na Mola wao.(Rejea Qur'aan Tukufu, Sura ya 3 (Surat Aali Imraan, Aya 169 kuwa: " *Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti (wafu). Bali hao ni wahai (watu hai), wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi "*
Kadhalika, imani kuwa maiti hurudishiwa roho zao na kuwa na maisha maalumu yaitwayo " *maisha ya Barzakh* " inashadidia dhana ya aliyekufa kuitwa ' *hayati*'.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)