MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI'

Neno *firasha* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]*  yenye maana ya aina ya godoro jembamba linalotengenezwa kwa vipande vya vitambaa.

Neno *firashi* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]*  yenye maana ya mbao ndogondogo zinazotumika kuunda mashua au jahazi.

Katika lugha ya Kiarabu, maneno *firasha* na *firashi* yanatokana na nomino ya Kiarabu  *firaashun/firaashan/firaaashin فراش*  yenye maana zifuatazo:

1. Kinachotandikwa ili kulala juu yake; godoro.

2. Kiota cha ndege.

3. Sehemu ya chini ya ulimi.

4. Makazi ya mtu; nyumba.

Mbali ya maana hizi nne, neno hili la Kiarabu lina maana tofauti zipatazo kumi na moja.

Kinachodhihiri ni kuwa maneno *firasha* na *firashi* ambayo katika Kiswahili ni maneno mawili yenye maana tofauti, katika lugha ya Kiarabu ni neno moja tu lenye maana anuai.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)