ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI' (/showthread.php?tid=2446) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI' - MwlMaeda - 03-05-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'FIRASHA' NA 'FIRASHI' Neno *firasha* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya aina ya godoro jembamba linalotengenezwa kwa vipande vya vitambaa. Neno *firashi* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana ya mbao ndogondogo zinazotumika kuunda mashua au jahazi. Katika lugha ya Kiarabu, maneno *firasha* na *firashi* yanatokana na nomino ya Kiarabu *firaashun/firaashan/firaaashin فراش* yenye maana zifuatazo: 1. Kinachotandikwa ili kulala juu yake; godoro. 2. Kiota cha ndege. 3. Sehemu ya chini ya ulimi. 4. Makazi ya mtu; nyumba. Mbali ya maana hizi nne, neno hili la Kiarabu lina maana tofauti zipatazo kumi na moja. Kinachodhihiri ni kuwa maneno *firasha* na *firashi* ambayo katika Kiswahili ni maneno mawili yenye maana tofauti, katika lugha ya Kiarabu ni neno moja tu lenye maana anuai. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |