02-17-2022, 06:09 AM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUADI/AJWADI'
Neno *ajuadi/ajwadi* katika lugha ya Kiswahili ni *kivumishi* chenye maana zifuatazo:
1. -enye umaarufu sana, mashuhuri, -enye heshima kubwa.
2. -enye ubora zaidi.
3. -enye moyo wa kupenda kusaidia kwa hali na mali bila ubaguzi; karimu.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajuadi/ajwadi*( *soma: ajwadu/ajwada/ اجود )* lina maana zifuatazo:
1. Mtu karimu sana.
2. Mwenye kufanya kitu bora zaidi.
3. Mwenye kwenda kasi sana aghalabu farasi.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili la Kiarabu *ajwadu/ajwada/ اجود* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajuadi/ajwadi* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu hazikubadilika.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda