ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUADI/AJWADI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUADI/AJWADI' (/showthread.php?tid=2401) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUADI/AJWADI' - MwlMaeda - 02-17-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AJUADI/AJWADI' Neno *ajuadi/ajwadi* katika lugha ya Kiswahili ni *kivumishi* chenye maana zifuatazo: 1. -enye umaarufu sana, mashuhuri, -enye heshima kubwa. 2. -enye ubora zaidi. 3. -enye moyo wa kupenda kusaidia kwa hali na mali bila ubaguzi; karimu. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *ajuadi/ajwadi*( *soma: ajwadu/ajwada/ اجود )* lina maana zifuatazo: 1. Mtu karimu sana. 2. Mwenye kufanya kitu bora zaidi. 3. Mwenye kwenda kasi sana aghalabu farasi. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili la Kiarabu *ajwadu/ajwada/ اجود* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ajuadi/ajwadi* maana zake katika lugha ya asili - Kiarabu hazikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |