MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'MBASHARA/MUBASHARA' NA 'MUBASHIRI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'MBASHARA/MUBASHARA' NA 'MUBASHIRI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'MBASHARA/MUBASHARA' NA 'MUBASHIRI'

Neno *mbashara* katika lugha ya Kiswahili ni *kivumishi*  chenye maana ya kinachorushwa hewani moja kwa moja na kusikika na kuonwa wakati huohuo aghalabu kupitia matangazo ya redio na televisheni.
Mfano: Kipindi mbashara cha televisheni kitarushwa saa moja kamili usiku.

Katika lugha ya Kiarabu, neno linalofanana na hili kimuundo ni neno la Kiarabu  *mubaashara* *( *soma: mubaasharatun/mubaasharatan/mubaasharatin مباشرة)* tendo-jina ( *masw-dar مصدر* ) litokanalo na kitenzi cha Kiarabu *baashara باشر*  chenye maana zifuatazo:

1. Ameanza jambo au shughuli yeye mwenyewe bila ya kumtegemea mwengine.

2. Amedhihiri.

3. Amewahi kufanya tendo fulani; mara moja.

Neno *mubashiri* (Soma: *mubaashirun/mubaashiran/mubaashirin  مباشر*)  katika lugha ya Kiarabu ni jina la mtendaji ( *faailun فاعل* ) wa *kitenzi* cha Kiarabu *baashara باشر* lenye maana zifuatazo:

1. Kitu kinachotokea bila ya kusaidiwa na kitu kingine: *sababun mubaashir سبب مباشر* sababu ya moja kwa moja.

2. Amezungumza kwa kutumia data/nyaraka rasmi.

3. Matangazo ya moja kwa moja ya redio na televisheni *bath-thun mubaashir  بث مباشر.*

4. Uhusiano wa moja kwa moja usiokuwa na mtu wa kati. *Alaaqatun mubaashiratun علاقة مباشرة.*

5. Kodi isiyo ya moja kwa moja *dhwaribatun ghayru mubaashiratin ضريبة غير مباشرة* kama kodi inayopatikana kutokana na mauzo ya stampu.

Kinachodhihiri ni kuwa Waswahili wamelichukua neno la Kiarabu *mubaasharatun    مباشرة* wakalitohowa kuwa *mbashara* na kulipa maana ya neno la Kiarabu *mubaashirun/mubaashiran/mubaashirin مباشر* ambalo moja ya maana zake ni matangazo ya moja kwa moja aghalabu kupitia redio na televisheni.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)