MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA'

Neno *karibu* katika lugha ya Kiswahili ni *kielezi* chenye maana zifuatazo:

1. -a karibu na muda, -siokuwa ya zamani, -siochukua muda mrefu kutokea.

2. -siokuwa mbali na eneo.

3. -a chupuchupu; almanusura.

4. -siokuwa mbali kwa idadi; kiwango cha kukadiria.
Mfano: Walihudhuria watu karibu 1000.
Msemo: Karibu aangukie pua: Nusura adhurike.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *karibu* ni nomino ya Kiarabu  *qariibun/qariiban/qariibin قريب* yenye maana zifuatazo:

1. Sio mbali.

2.  Muda mfupi uliopita

3. Muda mfupi ujao.

4. Mwenye ukaribu wa nasaba/ukoo; jamaa/ndugu.

Neno *akaraba* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [Ngeli: a-/wa-] yenye maana zifuatazo:

1. Ndugu wa karibu kwa upande wa kuumeni au kuukeni.
Mfano: Mnuta ni akaraba wangu wa kuumeni.

2. Mtu wa familia yako wa ukoo mmoja nawe; jamaa yako.

Katika lugha ya Kiarabu, neno *akaraba* limekopwa kutoka neno la Kiarabu *aqribaau* (soma: *aqribaau/aqribaa-a اقرباء* ) ambalo ni nomino wingi wa neno karibu (soma: *qariibun/qariiban/qariibin قريب*) lenye maana ya ndugu/jamaa wa mtu *aqribaaul Insaani اقرباء الإنسان* .

Kinachodhihiri ni kuwa Waswahili wamelichukua neno *karibu* (soma: *qariibun/qariiban/qariibin قريب* )  wakalifanya kielezi na kulipa maana kadhaa zinazokaribiana na maana zake katika lugha asili - Kiarabu na maana nyinginezo huku wakiacha maana yake ya *ndugu wa karibu* na kisha wakalichukua neno *akaraba* linalotokana na neno *aqribaau* lililo wingi wa neno *karibu (qariibun  قريب)* wakalipa maana za neno *qariibun قريب* katika lugha ya Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)