ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA' (/showthread.php?tid=2384) |
ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA' - MwlMaeda - 02-02-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'KARIBU' NA 'AKARABA' Neno *karibu* katika lugha ya Kiswahili ni *kielezi* chenye maana zifuatazo: 1. -a karibu na muda, -siokuwa ya zamani, -siochukua muda mrefu kutokea. 2. -siokuwa mbali na eneo. 3. -a chupuchupu; almanusura. 4. -siokuwa mbali kwa idadi; kiwango cha kukadiria. Mfano: Walihudhuria watu karibu 1000. Msemo: Karibu aangukie pua: Nusura adhurike. Katika lugha ya Kiarabu, neno *karibu* ni nomino ya Kiarabu *qariibun/qariiban/qariibin قريب* yenye maana zifuatazo: 1. Sio mbali. 2. Muda mfupi uliopita 3. Muda mfupi ujao. 4. Mwenye ukaribu wa nasaba/ukoo; jamaa/ndugu. Neno *akaraba* katika lugha ya Kiswahili ni nomino [Ngeli: a-/wa-] yenye maana zifuatazo: 1. Ndugu wa karibu kwa upande wa kuumeni au kuukeni. Mfano: Mnuta ni akaraba wangu wa kuumeni. 2. Mtu wa familia yako wa ukoo mmoja nawe; jamaa yako. Katika lugha ya Kiarabu, neno *akaraba* limekopwa kutoka neno la Kiarabu *aqribaau* (soma: *aqribaau/aqribaa-a اقرباء* ) ambalo ni nomino wingi wa neno karibu (soma: *qariibun/qariiban/qariibin قريب*) lenye maana ya ndugu/jamaa wa mtu *aqribaaul Insaani اقرباء الإنسان* . Kinachodhihiri ni kuwa Waswahili wamelichukua neno *karibu* (soma: *qariibun/qariiban/qariibin قريب* ) wakalifanya kielezi na kulipa maana kadhaa zinazokaribiana na maana zake katika lugha asili - Kiarabu na maana nyinginezo huku wakiacha maana yake ya *ndugu wa karibu* na kisha wakalichukua neno *akaraba* linalotokana na neno *aqribaau* lililo wingi wa neno *karibu (qariibun قريب)* wakalipa maana za neno *qariibun قريب* katika lugha ya Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |