MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA'

Neno *rubaa* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-]*  yenye maana zifuatazo:

1. Jumuiya ya watu wanaoishi na wanaofanya kazi pamoja kwa sababu wana uhusiano fulani unaowaunganisha; Watu wengi wanaofanya kazi pamoja kwa kuunganishwa na uhusiano fulani.

2.  Kitendo cha kuweka mguu mmoja juu ya mwengine hali ukiwa umekaa.
*Mfano* : Mgeni alipopewa kiti alikaa rubaa.

3. Uwanja au uga wa shughuli fulani.
*Mfano* : Jangala siku hizi ni maarufu katika rubaa za michezo.

4. Kikundi cha askari wanaopangiwa na kutekeleza majukumu yao chini ya kiongozi mmoja.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *rubaa*( *soma: rubaau/rubaa-a رباع )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana ya kukariri namba 4: nne nne/wanne wanne. Kwa mfano: *Hum Jaauu Rubaa-a هم جاءوا رباعا* Wamekuja wanne wanne.

Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *rubaa-a رباعا* lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa nomino ya Kiswahili ' *rubaa* ' lilibeba maana mpya.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)