ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA' (/showthread.php?tid=2379) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA' - MwlMaeda - 01-29-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'RUBAA' Neno *rubaa* katika lugha ya Kiswahili ni *nomino: [Ngeli: i-/zi-]* yenye maana zifuatazo: 1. Jumuiya ya watu wanaoishi na wanaofanya kazi pamoja kwa sababu wana uhusiano fulani unaowaunganisha; Watu wengi wanaofanya kazi pamoja kwa kuunganishwa na uhusiano fulani. 2. Kitendo cha kuweka mguu mmoja juu ya mwengine hali ukiwa umekaa. *Mfano* : Mgeni alipopewa kiti alikaa rubaa. 3. Uwanja au uga wa shughuli fulani. *Mfano* : Jangala siku hizi ni maarufu katika rubaa za michezo. 4. Kikundi cha askari wanaopangiwa na kutekeleza majukumu yao chini ya kiongozi mmoja. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *rubaa*( *soma: rubaau/rubaa-a رباع )* ni nomino ya Kiarabu yenye maana ya kukariri namba 4: nne nne/wanne wanne. Kwa mfano: *Hum Jaauu Rubaa-a هم جاءوا رباعا* Wamekuja wanne wanne. Kinachodhihiri ni kuwa neno la Kiarabu *rubaa-a رباعا* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa nomino ya Kiswahili ' *rubaa* ' lilibeba maana mpya. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |