01-19-2022, 02:33 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI'
Neno aharishauri katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/-wa] yenye maana ya kundi la wanachama wenye malengo maalumu; wajumbe.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aharishauri( soma: ahlush - shuraa اهل الشورى ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:
1. Watu waliopewa mamlaka na madaraka ya kushauriana na kukata shauri/kupitisha uamuzi.
2. Neno shuraa likitanguliwa na neno majlis , hubeba maana ya baraza la ushauri ; bunge majlisush shuraa مجلس الشورى.
3. Jambo la kushauriana.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahlush shuraa/shawri lilipoingia katika Kiswahili lilibadilika kuwa aharishauri na kuchukua maana mpya ya kundi la wanachama wenye malengo maalumu; wakumbe.
Shukran sana.
Khamis S.M. Mataka.

Mwl Maeda