MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AHARISHAURI'

Neno aharishauri katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: a-/-wa] yenye maana ya kundi la wanachama wenye malengo maalumu; wajumbe.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aharishauri( soma: ahlush - shuraa اهل الشورى ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Watu waliopewa mamlaka na madaraka ya kushauriana na kukata shauri/kupitisha uamuzi.

2. Neno shuraa likitanguliwa na neno majlis , hubeba maana ya baraza la ushauri ; bunge majlisush shuraa مجلس الشورى.

3. Jambo la kushauriana.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ahlush shuraa/shawri lilipoingia katika  Kiswahili lilibadilika kuwa aharishauri na kuchukua maana mpya ya kundi la wanachama wenye malengo maalumu; wakumbe.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.