MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA
#1
MOFOfONOLOJIA (MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA)
Mofofonolojia ni taaluma inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.
Mfano
v  Utendea Panga>  pangia
Funga>  fungia       a,i,u
Piga>   pigia
Cheza>  chezea
Soma>   Somea         e,o
Zoa>    zolea
Mofofonolojia huzalisha kanuni ambazo zinaelezea mazingira ya utokeaji wa mofu na alomofu zake.
KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA
Kanuni hizi huelezea maathiriano ya kifonolojia yanayoathiri mofolojia ya maneno na jinsi badiliko la kimofofonolojia la neno linavyoelezeka kikanuni.
Kanuni hizi husaidia kujua jinsi maneno yanavyobadilika toka muundo ndani wa neno hadi muundo nje wa neno.
Kanuni za kimofofonolojia hutawaliwa na sifa zifuatazo
  1. Kanuni za kifonolojia hazina vighairi mfano; hakuna vighairi katika kanuni ya kifonolojia isemayo mkazo katika Kiswahili huwekwa silabi ya pili kutoka mwishoni mwa neno.
  2. Kanuni za kimofofonolojia huwa na vighairi vingi; Kanuni hii huhusu lugha mahususi na hutumika  katika baadhi ya mofimu tu kwa mfano katika mofu ya utendea.
mfano
piga>  pigia
panga> pangia
funga> fungia
tenga> tengea
choma> chomea
//utendea//—–>i/-mz+[a,i,u]
——->e/-mz+[e,o]
AINA ZA KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA.
  1. Kanuni ya usilimisho
Kanuni hii inahusu maathiriano ya mofimu zinazofuatana. Maathiriano hayo huzifanya mofimu zifanane zaidi kuliko zikiwa pekee.
Mfano(1)
  1. a) n+goma—–>{ngoma}
  2. b) n+dizi——>{ndizi}
  3. c) n+buzi—–>{mbuzi}
  4. d) n+bingu—–>{mbingu}
n——>m/-k
Huo ni usilimisho wa nazali.
Mfano(2)
  1. a) n+refu—–>{ndefu}
  2. b) n+limi—->{ndimi}
r——>d/n-
l——->d/n-
Huo ni usilimisho wa konsonanti inayotanguliwa na nazali(N)
  1. Ukaakaishaji
Haya ni maathiriano ambayo sauti isiyo ya kaakaa gumu hulazimishwa  kuwa sauti ya kaakaa gumu.
Mfano
  1. a) ki+ama——->chama
  2. b) ki+ombo——->chombo
  3. c) ki+uma——–>chuma
  4. d) ki+eo——>cheo
ki——->ch/-i
  1. Udondoshaji
Mofimu hudondoshwa kutokana na mfuatano wa mofimu unaoleta maathiriano
Mfano
  1. a) wanasoma –hawasomi
  2. b) anasoma-hasomi
  3. c) nilikunywa-sikunywa
//njeo// ——-> θ/-ukanushi
 
  1. Uingizaji/uchopekaji
Mofimu huchopekwa kwenye mzizi ili kusaidia kuimarisha mzizi wa neno. Uchopekaji aghalabu hutokea kwenye mizizi ya silabi moja.
Mfano
  1. a) -j-       anakuja
  2. b) -nywa-    anakunywa     θ———>ku/-mz   -j,-nyw -,-f-
  3. c) -f-       atakufa
 
  1. Tangamano la irabu
Hapa irabu zinaathiriana na kuamua kutumia irabu moja (i, au
  1.   e) kuwakilisha baadhi ya mofimu.
Mfano
Panga – pangia
Piga  – pigia
funga – fungia
Cheza – chezea
Soma –  somea
//utendea//———>i/-mz-  a, i, u
———>e/-mz-   e, o
  1. Msinyao/mvutano wa irabu
Hutokea ambapo irabu ndefu hulazimishwa kutokea kama irabu fupi
na hivyo kuwa moja badala ya mbili.
Mfano
  1. a) wa+alimu – walimu
  2. b) wa+ema  – wema
  3. c) wa+izi  – wezi
a+a – a
a+e – e
a+i  – e
  1. Uyeyushaji
Ni uundaji wa sauti viyeyusho vitokanavyo na sauti irabu
   Mfano
Mu+ana – mwana
Ku+etu – kwetu
Vi+angu-vyangu
Mu+izi-mwizi
Vi+umba-vyumba
u——->w/-I,I # u
i——->y/-I,I # i
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)