MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Chuo (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=3) +---- Forum: Shahada (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=20) +----- Forum: Nukuu (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=22) +----- Thread: MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA (/showthread.php?tid=1619) |
MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA - MwlMaeda - 11-30-2021 MOFOfONOLOJIA (MIFANYIKO YA KIMOFOLOJIA)
Mofofonolojia ni taaluma inayoshughulikia uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofimu katika mfuatano wake.
Mfano
v Utendea Panga> pangia
Funga> fungia a,i,u
Piga> pigia
Cheza> chezea
Soma> Somea e,o
Zoa> zolea
Mofofonolojia huzalisha kanuni ambazo zinaelezea mazingira ya utokeaji wa mofu na alomofu zake.
KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA
Kanuni hizi huelezea maathiriano ya kifonolojia yanayoathiri mofolojia ya maneno na jinsi badiliko la kimofofonolojia la neno linavyoelezeka kikanuni.
Kanuni hizi husaidia kujua jinsi maneno yanavyobadilika toka muundo ndani wa neno hadi muundo nje wa neno.
Kanuni za kimofofonolojia hutawaliwa na sifa zifuatazo
mfano
piga> pigia
panga> pangia
funga> fungia
tenga> tengea
choma> chomea
//utendea//—–>i/-mz+[a,i,u]
——->e/-mz+[e,o]
AINA ZA KANUNI ZA KIMOFOFONOLOJIA.
Kanuni hii inahusu maathiriano ya mofimu zinazofuatana. Maathiriano hayo huzifanya mofimu zifanane zaidi kuliko zikiwa pekee.
Mfano(1)
n——>m/-k
Huo ni usilimisho wa nazali.
Mfano(2)
r——>d/n-
l——->d/n-
Huo ni usilimisho wa konsonanti inayotanguliwa na nazali(N)
Haya ni maathiriano ambayo sauti isiyo ya kaakaa gumu hulazimishwa kuwa sauti ya kaakaa gumu.
Mfano
ki——->ch/-i
Mofimu hudondoshwa kutokana na mfuatano wa mofimu unaoleta maathiriano
Mfano
//njeo// ——-> θ/-ukanushi
Mofimu huchopekwa kwenye mzizi ili kusaidia kuimarisha mzizi wa neno. Uchopekaji aghalabu hutokea kwenye mizizi ya silabi moja.
Mfano
Hapa irabu zinaathiriana na kuamua kutumia irabu moja (i, au
Mfano
Panga – pangia
Piga – pigia
funga – fungia
Cheza – chezea
Soma – somea
//utendea//———>i/-mz- a, i, u
———>e/-mz- e, o
Hutokea ambapo irabu ndefu hulazimishwa kutokea kama irabu fupi
na hivyo kuwa moja badala ya mbili.
Mfano
a+a – a
a+e – e
a+i – e
Ni uundaji wa sauti viyeyusho vitokanavyo na sauti irabu
Mfano
Mu+ana – mwana
Ku+etu – kwetu
Vi+angu-vyangu
Mu+izi-mwizi
Vi+umba-vyumba
u——->w/-I,I # u
i——->y/-I,I # i
|