MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MAISHA YA SHAABAN ROBERT NA MAWAZO YAKE (M.A. Maganga) – 2

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MAISHA YA SHAABAN ROBERT NA MAWAZO YAKE (M.A. Maganga) – 2
#1
[Image: shaabanrobert.jpg]
Bila shaka, baada ya kusoma
mawazo mengi ya Shaaban Robert juu ya maisha ya binadamu, mtu atakuwa na hamu
ya kutaka kujua maswali gani yeye mwenyewe alivyoishi. Na pengine atataka
kujiuliza maswali kama haya: Je, yeye mwenyewe Shaaban aliishije na jamaa zake?
Aliishi kwa kupendana, kusaidiana na kwa usawa wa ujamaa, kama ionekanavyo
katika Adili na Nduguze? Hayo ni
kuhusu maisha yake na jamaa yake. Lakini je, yeye binafsi aliishi kwa kufanya
kazi kwa bidii kadiri ya uwezo wake, na alijitegemea kama awaidhivyo katika Wasifu wa Siti Binti Saad? Je, mtu
akiyachunguza maisha yake ataona nini katika uhusiano wa uraia wake nan chi yake?
Majibu ya maswali ya namna hii ndiyo nipendayo tuyapekuepekue katika Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini. Siyo
kwamba mimi nataka kukariri au kufupisha maandishi ya kitabu chake, bali
natarajia kutoa maoni yangu kuhusu maisha yake, na kuyalinganisha na maoni yake
kuhusu maisha ya watu kwa ujumla.
Kama ilivyo sheria ya asili, mtu
huzaliwa na kufa. Na katikati ya hayo mambo mawili ndipo penye maisha ya mtu. Mambo
mengi yanaweza kutokea katika nafasi hiyo. Napenda kutumia neno hili ‘nafasi’
ili kuleta maana halisi kwamba maisha ya mtu ni nafasi hasa ya kutenda mambo
kadha wa kadha. Maisha ya mtu ndiyo nafasi yake, na matendo yote hutegemea
nafasi hiyo. Nafasi hii ina ncha, na kwa hivyo huisha. Kwa sababu hii, maisha
si kitu cha daima na milele. Yana ukomo wake.
Inaelekea kuwa Shaaban Robert
alijivika mawazo haya kichwani mwake. Lakini hapa pana jambo zima: nalo ni
kwamba hakukomea tu kuwaza kwamba maadamu maisha ni nafasi ya mtu basi ni
lazima mtu ayatumie vema kwa ajili yake binafsi. Marehemu aliona kwamba ingawa
mtu ndiye aliyepewa maisha, lakini maisha yenyewe ni kwa ajili ya maendeleo ya
nchi. Ikiwa basi ‘maisha ya mtu ni msingi wa maendeleo ya nchi’ ndiyo kusema
juu ya maisha machafu au mazuri? Maisha ya bidii ya kazi, au ya ulegevu na
uvivu? Maisha yenye mipango maalumu, au yale yajiendeayo yenyewe ovyo ovyo tu? Maisha
ya kibinafsi au maisha ya ujamaa?
Maisha ya marehemu ya miaka
ishirini na sita ya mwanzo hayakuendelezwa katika Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini kwani, kama asemavyo katika
utangulizi, hayo yaliandikwa katika insha ambayo haikupigwa chapa na ambayo
ilikuwa katika mwandiko wa mkono na kisha haikuwa na nakala. Kwa hivyo basi,
katika hiki, mambo hayo hayamo. Baada ya shindano, insha hiyo haikuonekana
tena. Hata hivyo, tuna ufununu kwamba hayo hasa yalikuwa maisha ya mwandishi
wakati wake wa utoto-alivyopenda kucheza na alivyocheza, alivyokwenda vyuoni na
kumbini hadi akawa mtu mzima, akapata kazi na kuoa. Maisha ya kwenda vyuoni na
kupata kazi hatimaye ni maisha ya aina ya siku za kisasa. Lakini hakuna mengi
ya kuyatolea maoni kwani tumepewa hayo kwa muhtasari tu.
Kwa hivyo, tuanzie mwaka wa
ishirini na saba wa maisha yake.
Muhtasari nilioutaja awali
haugusiijambo lolote kubwa ambalo Shaaban alilifanya kabla ya miaka hii
ishirini na saba. Watu wengi, kama hawajafanya lolote katika miaka yao ishirini
na mitano ya kwanza, hakukata tamaa kuwa hawataweza tena kufanya lolote kwa
sababu wamekuwa ‘wazee’ ati! Je, Shaaban Robert alijionaje alipokuwa na umri
huo? Anasema, ‘Maisha yalikuwa bado mapya na matumaini yake yalikuwa mengi sana.’
Alikuwa mzima wa afya na mwenye furaha moyoni. Anasema, ‘Nilikuwa katika mwanzo
tu wa maisha; bado sijafika katikati wala mwisho wake.’ Lakini hakuridhika kwa
zile ‘kurasa’ chache za maisha yake ya nyuma kwani hazikuandikwa yoyote yaliyo
azizi yawezayo ‘kuwatamanisha wengine kuyanakili’ wala mwenyewe hazikumridhisha
kwamba alitarajia maisha yake yawe ni kielelezo kwa wengine na, wawezao,
wayanakili. Hakukata tama kwani aliwaza kuwa pengine ubora wa mtu huwezekana
kuwa katika wakati ujao. Yaliyopita si ndwele; ganga yajayo. Kwa hivyo
alijiandaa kutumia nafasi yake.
Shaaban aliamini kuwa ipo bahati
na huwapata watu, lakini haiji tu hivi hivi-sharti mtu ajikongoje kuiendea
ndipo akutane nayo, au ainyoshee mkono kujaribu kuishika. Kwa kutokufanya hivi
watu wamezichelewesha bahati zao au pengine wamezikosa kabisa. Na bahati
haitokei mara kwa mara. Na hata kama ingetokea mara kwa mara maisha ya mtu ni
nafasi fupi iliyo na mwisho.
Akiwa na mawazo hayo juu ya
bahati, Shaaban akayapata maisha yake mpango maalum na akaweza kuzitandaza
fikra zake zote huku ana picha kamili ya nini atakacho. Katika mpango wa maisha
yake jambo moja alilitilia mkazo vilivyo: hakutaka utajiri au mamlaka juu ya
watu. Ingawa hivi vilileta fahari, lakini kwa wakati ule vitu hivi alivihofu. Msomaji
anaweza kukubaliana naye au kumpinga akijiuliza kuwa ile miaka ya 1936 ilikuwa
ni enzi gani? Jambo alilotarajia maishani mwake ni ‘jina lililo mbali na madoa
katika umaskini na unyonge.’ Kwa hivyo kama jambo hili lilikuwa jepesi au gumu,
zuri au baya, la kumpa mtu moyo au uchovu, heri lilinganishwe nay ale mengine
mawili kwa kufuata mazingira ya nchi ya Tanganyika siku hizo. Na alitarajia
kulipata hilo ‘jina’angalau nusu au hata robo yake.
Hebu sasa tumwangalie Shaaban
Robert akiwa mchumba, mume na mfiwa-kwani jambo la ndoa, ingawa si watu wote
wanaolitekeleza, ni mojawapo ya miinuko ionekanayo katika maisha ya mtu. ‘Kabla
ya kuoa nilitafuta umbo namna yake muda wa miaka kumi!’ Shaaban alikuwa
amemtafuta mke ambaye ‘uzuri wake ulikuwa kamili’ na kwa tabia alikuwa
mwaminifu na mfano wa kuiga katika nyumba. Mchanganyiko huu wa uzuri wa umbo,
pamoja na tabia ndio uliokuwa ‘jembe’ au ‘nyumba’ kwa maongezi ya uchaguzi wa
mke.
Baada ya kumwoa Amina mwenye sifa
zote hizo mbili, Shaaban alimpenda sana na kumshukuru kwamba alimsaidia katika
mambo mengi wakati wa maisha yao pamoja ambayo yeye pekee yangelimshinda
kuyatenda. Na mengi waliyatarajia kuyafanya pamoja, Shaaban na Amina, lakini
ugonjwa ulimnyakua mapema mkewe mpenzi na akamtangulia mumewe. Bwana Shaaban
hakukilalamikia kifo kwani alijua ni lazima kije; alilalamikia kuja kwake
mapema hivyo. Akalia machozi kama alivyomlilia marehemu babake na alizipamba
dua zake kwa shairi aliloombea marehemu mkewe akubaliwe peponi.
Methali yasema ‘akosaye la mama
la mbwa huamwa’. Shaaban alifahamu kuwa mwanawe na binti yake waliyakosa malezi
na adili zote za mama yao, ndipo akawapa usia katika tenzi ambazo zilitarajiwa
kuwaongoza katika maisha yao. Akatarajia kuwalea watoto wake na kuwafundisha
wema wa moyoni. Shaaban hakuwaacha watoto wake wakue tu hivi hivi kama ua mwitu
linalotanda ovyo bila kuongozwa. Yeye aliwatunza kama maua ya bustanini.
Utenzi wa Hati kwa bintiye na Utenzi
wa Adili kwa mwanawe zilikuwa fimbo au kamba zilizo imara na zilizoongoza
kukua  kwao na maisha yao. Alikuwa na
mengi ya kuwausia kuhusu dunia. Urefu wa kila utenzi ulikuwa beti mia moja. Kwa
ufupi alimwandikia bintiye usia wa kumuasa aitunze hiyo hati imsaidie katika
dunia ngumu na ulimwengu wenye adha, asiwasaliti watu, awe na matendo mema
kwani yote hupaazwa kwa Mungu, na hati hiyo iwe mali na nuru kwake, ashike dini
kwani ni mali ya roho, ajifunze elimu awe mtalamu wa kupambanua halali na
haramu, nyumba yake iwe nadhifu, taabu zikimkabili awe amejiandaa, nia ya
maendeleo aitie moyoni, na asingoje bahati imtendee yote, kwani: ‘watu wengi
huchelewa kwa kungoja kutendewa.’ Majivuno hayafai, asishiriki uwongo, masuto
si mazuri, awe na ulimi wa kulainisha na ulio mtamu, awe na cheko na tabasamu,
usoni awe na haya, awapende wote-wenye vyeo na wanyonge-naawe na adabu kwa baba
na mama na walio sawa nao, awe mlezi bora, ajifundishe kukinai, mapato yake
yawe halali, na waijenge dunia nzuri na ya furaha-yeye na mumewe.
Mtoto wake wa kiume vile vile
alimpa maagizo ya adili. Kwanza alimfundisha awe mcha Mungu, Muumba mbingu nan
chi, wanyama na ndege na samaki, na ajuaye yote kwa ghibu bila kusoma kitabu. Ampe
yeyote roho yake ili shetani asiiteke. Pili, amtii mkuu wa Serikali bila ya
kinyume. Tatu, awape taadhima baba na mama, awatendee kila jema. Nne, afanye
taaluma ya lugha. Tano, ajifunze elimu kwani:
‘Maisha bila elimu
Hayafai mwanadamu
Sababu mambo magumu
Mengi sana mbelee.

‘Milango wazi adimu
Kwa asiye na elimu
Kwa mwenye nayo gumu
Hujifungua wenyewe.’

 
Sita, akioa mke amshike kwa mapenzi bila makeke, awe na
msamaha kwake, ampe heshima kama mama wa watoto wake, awapende watoto wake,
awafunze taalimu na adili, awapende sana nduguze kama alivyofanya Adili,
apatane na masahibu, kwa rafiki zake awe kitu cha makumbuko akiwapo asiwepo,
ajenge matendo mema, awapende watu wote, afiche siri zake ila kwa wachache
wapasao, akiweka ahadi kutimiza ajitahidi, atoe msaada kwa wenye kulemewa,
asiwe mgomvi, awe na uso wenye tabasamu na wenye furaha, afanye kazi kwa bidii
bila uvivu, asahihishe makosa, amwombee dua babake ambaye ni Mwafrika
madhubuti. Hakika huo ndio usia wa kuwapa watoto majumbani kabla hawajaenda
vyuoni, kwani kuna methali isemayo ‘asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na
ulimwengu.’ Maagizo kama hayo ni tunu, ngao na mwangaza katika maisha.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)