MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA
#1
NI HERI NINGEKUROGA
Mara ngapi nakuonya, uwe wangu peke yangu,
Haya uliyoyafanya, yamenitia uchungu,
Vile nilivyokuonya, ni bure maneno yangu,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Sikuthubutu limbwata, moyo wako kuushika,
Niliepuka matata, usije ukawehuka,
Leo haya kunipata, na mimi nimegutuka,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Mara kadha niliwaza, nende kwa Kalumanzila,
Mawazo nikapuuza, chanzo cha haya madhila,
Sasa kimetua kiza, siwezi tena kulala,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Sasa mbali umekwenda, kurudi umekaidi,
Ili unitoe chonda, utimize makusudi,
Nimebakia kukonda, pamwe na zangu juhudi,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Yako simu ninapiga, haupokei mwendani,
Nimebaki kichwa boga, sijui nifanye nini,
Au chupa ningesaga, nitoweke duniani,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Nakumbuka ile juzi, na ulivyonitukana,
Umezidi siku hizi, tena mapenzi hakuna,
Nalia sitokwi chozi, ninabaki kujikuna,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Beti chache nasimama, sili ugali kushiba,
Unionee huruma, uchungu unanikaba,
Kwa raha imegoma, zimepita siku saba,
Kwa haya uliyofanya, ni heri ningekuroga.

Mtunzi Filieda Sanga Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
Mwl Maeda
Reply

Messages In This Thread
SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA - by MwlMaeda - 08-13-2021, 11:43 PM
RE: SHAIRI: NI HERI NINGEKUROGA - by MwlMaeda - 08-14-2021, 11:00 PM

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)