Pweke ndimi, na ukurasa bikira
Ni mnyemi, naudara hiudara
Hausemi, wala kutowa ishara!
‘Mekodowa, mato pasi kupepesa
Sawa sawa, umenyoka ukurasa
Umetuwa, japo ningaupapasa
Chamba: 'Nena, na mimi nakusikiza
Au guna, aula ninong’oneza
Umenuna ? Basi ngaa niapiza!'
Haujibu, utadhaniya ni mfu
Au bubu, tena kiziwi kipofu!
Wan’adhibu, kwake sijafuwa dafu!
Ha-u-maji, hasema taukamuwa
Si mkwiji, hasema taufunguwa
Siliwiji, la kutenda hapumuwa
Mkaidi, ukurasa umedinda!
Liso budi, ndilo la mtu kutenda
Nd’o narudi, na mtungi wangu shinda!
Abdilatif Abdalla
Ni mnyemi, naudara hiudara
Hausemi, wala kutowa ishara!
‘Mekodowa, mato pasi kupepesa
Sawa sawa, umenyoka ukurasa
Umetuwa, japo ningaupapasa
Chamba: 'Nena, na mimi nakusikiza
Au guna, aula ninong’oneza
Umenuna ? Basi ngaa niapiza!'
Haujibu, utadhaniya ni mfu
Au bubu, tena kiziwi kipofu!
Wan’adhibu, kwake sijafuwa dafu!
Ha-u-maji, hasema taukamuwa
Si mkwiji, hasema taufunguwa
Siliwiji, la kutenda hapumuwa
Mkaidi, ukurasa umedinda!
Liso budi, ndilo la mtu kutenda
Nd’o narudi, na mtungi wangu shinda!
Abdilatif Abdalla
Mwl Maeda