MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI' 

Neno *ami*  katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* yenye maana zifuatazo:

1. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mwanamume aliyezaliwa tumbo moja na baba.

2. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mwanamume anayependa umaridadi na kujinadi.

3. *Kihisishi*, neno linalotumika kumwita mtu aghalabu wa rika lolote badala ya jina lake.

Katika lugha ya Kiarabu neno *ami* linatokana na neno la Kiarabu  *ammu (soma: ammun/amman/ammin عم)* lenye maana zifuatazo:

1. Ndugu mwanamume aliyezaliwa tumbo moja na baba.

2. Kundi kubwa la watu.

3. Mtende mrefu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno *ammun  عم*  lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa  kuwa neno *ami* maana yake ya msingi katika lugha asili - Kiarabu haikubadilika bali Waswahili walilipa neno hili maana mpya ya *mwanamume anayependa umaridadi na kujinadi.* na *kihisishi cha kumwita mtu badala ya jina lake.* na kuacha maana zingine katika lugha asili - Kiarabu.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*
Mwl Maeda
Reply

Messages In This Thread
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI' - by MwlMaeda - 04-16-2022, 09:52 AM

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)