ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI' (/showthread.php?tid=2513) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI' - MwlMaeda - 04-16-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AMI' Neno *ami* katika lugha ya Kiswahili ni *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* yenye maana zifuatazo: 1. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mwanamume aliyezaliwa tumbo moja na baba. 2. *Nomino [Ngeli: a-/wa-]* mwanamume anayependa umaridadi na kujinadi. 3. *Kihisishi*, neno linalotumika kumwita mtu aghalabu wa rika lolote badala ya jina lake. Katika lugha ya Kiarabu neno *ami* linatokana na neno la Kiarabu *ammu (soma: ammun/amman/ammin عم)* lenye maana zifuatazo: 1. Ndugu mwanamume aliyezaliwa tumbo moja na baba. 2. Kundi kubwa la watu. 3. Mtende mrefu. Kinachodhihiri ni kuwa neno *ammun عم* lilipoingia katika Kiswahili na kutoholewa kuwa neno *ami* maana yake ya msingi katika lugha asili - Kiarabu haikubadilika bali Waswahili walilipa neno hili maana mpya ya *mwanamume anayependa umaridadi na kujinadi.* na *kihisishi cha kumwita mtu badala ya jina lake.* na kuacha maana zingine katika lugha asili - Kiarabu. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |