01-03-2022, 09:48 AM
SHAIRI: MKE WA PILI
Nauliza wahisani,wenye hekima kichwani
Maji yafika shingoni,wenzangu niambieni
Wala huu si utani,nawaeleza bayani
Nitumie njia gani,Mke kutakaongeza
Sheria imetutaka,mwisho wanne kuoa
Hili kwangu sina shaka,nafsi imetulia
ila kazi kutamka,mke kuweza mwambia
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Ukisema umwambie,mara awezajifia
Au mara achukie,nyumba huwezi ingia
Daima yeye alie,kazi atakuachia
Nitumie njia gani, mke kutakaongeza
Utapolifanya hilo,hapiki tena chakula
Kila ufanyalo silo,hugoma hata kulala
Utahisi upo selo,kama ulofungwa jela
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Au nifanye kwa siri,asijue asilani
Siku ikiwa dhahiri,taniona mtu gani
Hili lataka hodari,sio mgonjwa mwilini
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Ikiwa hujamwambia,vipi utamtoroka
Vipi utampangia, nyumbani ukitoweka
Au utamwongopea,hili lanipa mashaka
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Uongo haupendezi,na ukweli unauma
Hebu nipeni la wazi,ili nitunze heshima
Mke halimpendezi,hata iwe amesoma
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Mwisho natua kalamu,karatasi nafunika
Tunaosoma elimu,majibu yahitajika
Dini ya uislamu,lazima kufahamika
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Nauliza wahisani,wenye hekima kichwani
Maji yafika shingoni,wenzangu niambieni
Wala huu si utani,nawaeleza bayani
Nitumie njia gani,Mke kutakaongeza
Sheria imetutaka,mwisho wanne kuoa
Hili kwangu sina shaka,nafsi imetulia
ila kazi kutamka,mke kuweza mwambia
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Ukisema umwambie,mara awezajifia
Au mara achukie,nyumba huwezi ingia
Daima yeye alie,kazi atakuachia
Nitumie njia gani, mke kutakaongeza
Utapolifanya hilo,hapiki tena chakula
Kila ufanyalo silo,hugoma hata kulala
Utahisi upo selo,kama ulofungwa jela
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Au nifanye kwa siri,asijue asilani
Siku ikiwa dhahiri,taniona mtu gani
Hili lataka hodari,sio mgonjwa mwilini
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Ikiwa hujamwambia,vipi utamtoroka
Vipi utampangia, nyumbani ukitoweka
Au utamwongopea,hili lanipa mashaka
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Uongo haupendezi,na ukweli unauma
Hebu nipeni la wazi,ili nitunze heshima
Mke halimpendezi,hata iwe amesoma
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Mwisho natua kalamu,karatasi nafunika
Tunaosoma elimu,majibu yahitajika
Dini ya uislamu,lazima kufahamika
Nitumie njia gani,mke kutakaongeza
Mwl Maeda