SHAIRI: MKE WA PILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MKE WA PILI (/showthread.php?tid=1959) |
SHAIRI: MKE WA PILI - MwlMaeda - 01-03-2022 SHAIRI: MKE WA PILI Nauliza wahisani,wenye hekima kichwani Maji yafika shingoni,wenzangu niambieni Wala huu si utani,nawaeleza bayani Nitumie njia gani,Mke kutakaongeza Sheria imetutaka,mwisho wanne kuoa Hili kwangu sina shaka,nafsi imetulia ila kazi kutamka,mke kuweza mwambia Nitumie njia gani,mke kutakaongeza Ukisema umwambie,mara awezajifia Au mara achukie,nyumba huwezi ingia Daima yeye alie,kazi atakuachia Nitumie njia gani, mke kutakaongeza Utapolifanya hilo,hapiki tena chakula Kila ufanyalo silo,hugoma hata kulala Utahisi upo selo,kama ulofungwa jela Nitumie njia gani,mke kutakaongeza Au nifanye kwa siri,asijue asilani Siku ikiwa dhahiri,taniona mtu gani Hili lataka hodari,sio mgonjwa mwilini Nitumie njia gani,mke kutakaongeza Ikiwa hujamwambia,vipi utamtoroka Vipi utampangia, nyumbani ukitoweka Au utamwongopea,hili lanipa mashaka Nitumie njia gani,mke kutakaongeza Uongo haupendezi,na ukweli unauma Hebu nipeni la wazi,ili nitunze heshima Mke halimpendezi,hata iwe amesoma Nitumie njia gani,mke kutakaongeza Mwisho natua kalamu,karatasi nafunika Tunaosoma elimu,majibu yahitajika Dini ya uislamu,lazima kufahamika Nitumie njia gani,mke kutakaongeza |