12-16-2021, 08:08 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' BALAGHAMU'
Neno balaghamu katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa; kikohozi kizito chenye utelezi anachotoa mtu anayeumwa aghalabu na kifua Kikuu au homa.
2. Hasira (hutumika katika msemo: 'Toa balaghamu zako; to hasira zako.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili balaghamu (soma: balghamun/balghaman/balghamin بلغم ) lina maana zifuatazo:
1. Kohozi: mate yaliyochanganyika na kamasi ambayo hutoka kwenye njia ya upumuaji.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili (balghamun بلغم) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *balaghamu* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika.
Shukran sana.
Khamis S.M. Mataka.

Mwl Maeda