MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI - ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU'

JIFUNZE KISWAHILI

Full Version: ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHAMU'
You're currently viewing a stripped down version of our content. View the full version with proper formatting.
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' BALAGHAMU'

Neno balaghamu katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mate mazito yanayokuwa kooni ambayo hutoka mtu anapokohoa; kikohozi kizito chenye utelezi anachotoa mtu anayeumwa aghalabu na kifua Kikuu au homa.

2. Hasira (hutumika katika msemo: 'Toa balaghamu zako; to hasira zako.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili balaghamu (soma: balghamun/balghaman/balghamin بلغم ) lina maana zifuatazo:

1. Kohozi: mate yaliyochanganyika na kamasi ambayo hutoka kwenye njia ya upumuaji.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili (balghamun بلغم) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *balaghamu* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.