12-15-2021, 02:28 PM
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA'.
Neno muktadha (wingi: miktadha) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mazingira yanayobainisha mahali jambo lilipofanyika.
2. Mazingira ya neno (msamiati) katika tungo au sentensi yanayoonesha uhusiano wake na maneno mengine.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *muktadha* ( soma: *muqtadhwaa* *مقتضى* ) lina maana zifuatazo:
1. Kinachohitajika/kinacholazimu; jina la Mtendewa wa kitenzi cha Kiarabu iqtadhwaa اقتضى (-،mehitaji, -melazimu.)
2. Mazingira ya jambo fulani.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *muqtadhwaa* *مقتضى* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *muktadha* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*

Mwl Maeda