MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 02*

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 02*
#1
SIMULIZI: “JENEZA
LA AJABU “
**SEHEMU YA 02*
Ikulu kwa mfalme;
Ngome ya mfalme
inakumbwa na majonzi mazito ,kutokana na hali ya mfalme kuwa mbaya sana. Wapo
waliofurahi kumuona katika hali ile, hasa wananchi wake ambao hawakupendezwa na
uongozi wake huku wakitamani afe haraka, waweze kuwa huru kutoka katika taabu
na mateso yaliyosababishwa na uongozi wake wa kikatili wa mfalme Mutapa. Lakini
wachache walihuzunika sana, hasa watoto wake pamoja na wake zake mfalme, huku
wakimuomba Mungu amuepushe na umauti.
“Mfalme mimi
ninaondoka kurudi nyumbani, lakini zingatia yale yote niliyokuambia, kwani kama
unavyoiona hali yako inazidi kuwa mbaya, usipokuwa makini mali zako na ufalme
wako utakwenda na maji “,asubuhi na mapema, mganga kutoka katika ardhi ya
Mwamuyeshi, akiwa ameshika kila kitu kwa ajili ya safari yake ya kurudi
nyumbani, anamuaga mfalme huku akimsisitiza kuzingatia maelekezo aliyompatia na
kisha kupanda farasi na kuondoka, huku akiongozana na askari wawili aliokuja
nao kwa ajili ya kumlinda njiani, askari waliotoka katika ngome ya mfalme
Muyeshi.
Mfalme Mutapa akitikisa
kichwa chake kuashiria kukubaliana na maelekezo ya mganga, na kumshuhudia
akitokomea mbele ya uso wake, anaamua kutoa amli kwa kutumia maandishi Njoshi
kufika ikulu haraka sana, kwani mfalme alishindwa hata kuzungumza hali
iliyowatia hofu watoto wa mfalme pamoja na wakeze.
“Baba nakuomba
usimdhuru Njoshi kwa chochote kile, lolote baya likimtokea sitajali hali yako
mbaya uliyonayo, nitakuua “,Grace aliongea huku akionesha kumaanisha kwa
maneno aliyoyazungumza, bila kujali ni kiasi gani alimpenda baba yake aliapa
kumtoa roho kwa mikono yake, kama tu kipenzi chake Njoshi akidhurika na jambo
lolote   na kuacha familia nzima ya
mfalme ikiwa midomo wazi, kwani hawakuamini maneno yale kama yalitoka kinywani
kwa Grace, msichana aliyependwa sana na mfalme.
“Hahaa, sasa mpaka
wewe unamuua baba, sisi tutakua wapi, labda uanze kutuua sisi “,Kijana
mkubwa wa mfalme, kijana ambaye Mutapa alimuamini sana na kumuahidi kumrithisha
ufalme na mali zake, kutokana na uhodari wake alizungumza kwa kejeli, na
kupelekea familia nzima kucheka na kusahau hali mbaya ya mfalme aliyokuwa nayo.
Ghafla mfalme alitoa
amli ya familia nzima kukaa kimya kwa kutumia ishara, huku akitaka agizo la
Njoshi kufika ikulu, litekelezwe mala moja bila kujali onyo kali alilopokea
kutoka kwa binti yake Grace, mtoto pekee wa kike aliyempenda sana.
Nyumbani kwa kina
Njoshi;
Ilikua siku ya jumatatu
asubuhi, kama kawaida Njoshi hufanya mazoezi makali katika siku hii kwani wiki
nzuri huonekana siku hii, hivyo aliamini akifanya vizuri mazoezi siku ya
jumatatu, atakuwa fiti wiki nzima. Aliamka saa kumi na moja asubuhi, na kuanza
mazoezi ya kukimbia, siku zote alipenda kukimbia huku akiimba, kwani alikatiza
mitaa karibu yote ya nchi ndogo ya Mwamutapa, bila kujitambua kwani nyimbo
alizoimba zilimtia moyo na kumuondolea uchovu. “Ngoja nikimbie, nikimaliza
nije kunyenyua vyuma, ukombozi sio lelemama lazima wachache tuumie
“,Njoshi aliongea kwa ujasiri huku akitamani siku moja aweze kuishika nchi
na yeye kuwa mfalme, huku Grace akiwa malikia, kwani msichana mrembo Grace
alipendwa sana na wananchi na aliwaokoa mala nyingi walipokuwa wakionewa na
baba yake pamoja na kaka zake, kwani aliwaombea msamaha na kusikilizwa.
Walimuona kama ndio kondoo pekee aliyeishi ndani ya kundi la simba. Njoshi
alizidi kukimbia lakini bila kutegemea alijikuta akiishiwa na pumzi haraka sana
tofauti na siku zingine, bila kupoteza muda aliamua kurudi nyumbani kufanya
mazoezi mengine. “Mwanangu kweli wewe ni shujaa, natamani ndoto zako
zitimie nikiwa hai nishuhudie ukiwakomboa Wanamutapa wote “,ilikua tayali
imeshafika saa moja asubuhi, mama yake Njoshi aliweza kuamka na kumkuta mwanae
akiendelea na mazoezi, na kuzungumza maneno makali yaliyomshitua sana Njoshi,
haikuwa kawaida kwa mama yake kumwambia maneno mazito kiasi kile.
Njoshi alisitisha
mazoezi na kisha kutaka kumuulza mama yake, kwanini alizungumza vile, kwanini
mama yake asishuhudie ukombozi ambao mwanae alikuwa akiupanga, mama yake kaona
nini mbeleni katabili nini. Njoshi alizidi kujiuliza maswali kichwani mwake,
huku akimsogelea mama yake, mke wa marehemu Nyangoma, mganga na mtabili
aliyekuwa akitegemewa sana na mfalme Mutapa. Kutokana na kutabili kuwa ipo siku
mfalme atamuua kikatili bila kujali mema yote aliyomfanyia, aliamua kumfundisha
uganga na utabili mke wake, ili siku akifa mke wake aweze kurithi mikoba.
“Mwanangu Njoshi
Nyangoma, naona hatari kubwa iko mbele yako, utasafiri safari ndefu yenye visa
na mikasa ya ajabu ,mkanda huu mweusi na panga hili ndio siraha yako kuu,
iliyomuwezesha baba yako kutoka salama katika msitu wa majini, usikatae kwenda
huko, huko ndipo utaupata ufalme wa nchi hii, lakini ukirudi nyumbani utakuta
kabuli langu, mimi nikiwa tayali nimeshakuwa mifupa “,mama Njoshi
alizungumza kwa uchungu sana huku machozi yakimtoka, na kumkabidhi mwanae begi
dogo jeusi,kwani ndio ulikuwa mwisho wa kuonana yeye na mwanae mpendwa Njoshi.
“Sikuelewi mama
unaongea nini, mimi msituni huko niende kufanya nini sasa, kwanza huwezi kufa
mimi nitakulinda mpaka dakika ya mwisho “,Njoshi aliongea huku akimfuta
mama yake machozi, huku mama yake akiukumbuka ule msemo wa wahenga, msemo ambao
ulikua maarufu sana enzi zile afrika ikitawaliwa na wazungu, msemo uliosema
jambo usilo lijua ni kama usiku wa giza.
Njoshi akiwa
amemkumbatia mama yake, akizidi kumbembeleza aweze kunyamanza, alishangaa kuona
kundi kubwa la vijana shupavu, likiwa limevalia bukta fupi nyeusi, pamoja na
ngozi ya chui, huku mikononi wakiwa wameshika mikuki na kila aina ya siraha za
kivita, bila shaka aliweza kuwatambua, lilikuwa ni jeshi la mfalme Mutapa.
“Aiweeeeeeh
………Njoshi, aiweeeeh ………”,askari wale waliweza kumsalimu Njoshi, na
kumfanya mama yake kuacha kumkumbatia mwanae na kushuhudia watu wale
waliomsalimia mwanae. “Aiweeeeeh ………askari waaminifu wa mfalme wangu wa
ardhi ya Mwamutapa, niwasaidie nini? “,Njoshi aliitikia salamu kwa upole
na hekima, huku akiificha hasira yake na kisasi kizito kilicho rohoni mwake,
kutokana na baba yake kuuawa kikatili na mfalme.
Kwa upande wa mama yake
hakushangaa chochote, kwani alikwishaona kila kitu kitakachotokea mbele, na pia
siri ya mfalme ambayo wananchi hawakutakiwa kuifahamu, kuhusu kuzikwa mala
atakapokufa na kisha kufufuka bila wananchi kutambua chochote, ili aweze kuishi
na kutawala milele.
“Tumekuletea
ujumbe huu wa maandishi kutoka kwa mfalme, mkwe wako tafadhali pokea ……iweeeeh
“askari wale waliongea huku, mmoja aliyeonekana kuwa na cheo kikubwa kuwazidi
wenzake kutokana na kuvaa ngozi ya simba, ngozi iliyokuwa ikivaliwa na kila
kiongozi wa nchi ya Mwamutapa, akimkabidhi Njoshi karatasi yenye maandishi na
kisha kuisoma.
“Iweeeeeh …mkwe
wangu, nakuomba katika ikulu yangu, ninashida na wewe, nataka tuwekeane mkataba
ili uweze kumuoa binti yangu Grace “,Njoshi alisoma maneno yale na kisha
kutabasamu, tabasamu ambalo liliwafanya askari wale wa mfalme kuangaliana na
kisha kukonyezana, hali iliyoonesha kutambua siri fulani iliyokuwa imefichika.
“Mama peleka begi
hili ndani, mimi ngoja nikaonane na mfalme “,Njoshi aliongea huku
akionekana kufurahia sana, kwani hakuamini kama ipo siku mfalme atamtamkia kuwa
yeye ni mkwe wake,kwani siku zote aliambulia matusi na kutishiwa kifo,
alipoingia anga za mfalme Mutapa.
“Hapana mwanangu,
kama unanipenda, naomba hilo begi lisitoke mgongoni mwako “,mama yake
Njoshi aliongea huku akiwa na huzuni moyoni, huku akijaribu kutabasamu kuficha
huzuni yake, kwani huo ndio ulikuwa ni mwisho wa kuonana na mwanae katika ulimwengu
huu.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)