SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 02* - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Hadithi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=48) +---- Thread: SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 02* (/showthread.php?tid=963) |
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 02* - MwlMaeda - 08-21-2021 SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU “ **SEHEMU YA 02*
Ikulu kwa mfalme;
Ngome ya mfalme
inakumbwa na majonzi mazito ,kutokana na hali ya mfalme kuwa mbaya sana. Wapo waliofurahi kumuona katika hali ile, hasa wananchi wake ambao hawakupendezwa na uongozi wake huku wakitamani afe haraka, waweze kuwa huru kutoka katika taabu na mateso yaliyosababishwa na uongozi wake wa kikatili wa mfalme Mutapa. Lakini wachache walihuzunika sana, hasa watoto wake pamoja na wake zake mfalme, huku wakimuomba Mungu amuepushe na umauti. “Mfalme mimi
ninaondoka kurudi nyumbani, lakini zingatia yale yote niliyokuambia, kwani kama unavyoiona hali yako inazidi kuwa mbaya, usipokuwa makini mali zako na ufalme wako utakwenda na maji “,asubuhi na mapema, mganga kutoka katika ardhi ya Mwamuyeshi, akiwa ameshika kila kitu kwa ajili ya safari yake ya kurudi nyumbani, anamuaga mfalme huku akimsisitiza kuzingatia maelekezo aliyompatia na kisha kupanda farasi na kuondoka, huku akiongozana na askari wawili aliokuja nao kwa ajili ya kumlinda njiani, askari waliotoka katika ngome ya mfalme Muyeshi. Mfalme Mutapa akitikisa
kichwa chake kuashiria kukubaliana na maelekezo ya mganga, na kumshuhudia akitokomea mbele ya uso wake, anaamua kutoa amli kwa kutumia maandishi Njoshi kufika ikulu haraka sana, kwani mfalme alishindwa hata kuzungumza hali iliyowatia hofu watoto wa mfalme pamoja na wakeze. “Baba nakuomba
usimdhuru Njoshi kwa chochote kile, lolote baya likimtokea sitajali hali yako mbaya uliyonayo, nitakuua “,Grace aliongea huku akionesha kumaanisha kwa maneno aliyoyazungumza, bila kujali ni kiasi gani alimpenda baba yake aliapa kumtoa roho kwa mikono yake, kama tu kipenzi chake Njoshi akidhurika na jambo lolote na kuacha familia nzima ya mfalme ikiwa midomo wazi, kwani hawakuamini maneno yale kama yalitoka kinywani kwa Grace, msichana aliyependwa sana na mfalme. “Hahaa, sasa mpaka
wewe unamuua baba, sisi tutakua wapi, labda uanze kutuua sisi “,Kijana mkubwa wa mfalme, kijana ambaye Mutapa alimuamini sana na kumuahidi kumrithisha ufalme na mali zake, kutokana na uhodari wake alizungumza kwa kejeli, na kupelekea familia nzima kucheka na kusahau hali mbaya ya mfalme aliyokuwa nayo. Ghafla mfalme alitoa
amli ya familia nzima kukaa kimya kwa kutumia ishara, huku akitaka agizo la Njoshi kufika ikulu, litekelezwe mala moja bila kujali onyo kali alilopokea kutoka kwa binti yake Grace, mtoto pekee wa kike aliyempenda sana. Nyumbani kwa kina
Njoshi; Ilikua siku ya jumatatu
asubuhi, kama kawaida Njoshi hufanya mazoezi makali katika siku hii kwani wiki nzuri huonekana siku hii, hivyo aliamini akifanya vizuri mazoezi siku ya jumatatu, atakuwa fiti wiki nzima. Aliamka saa kumi na moja asubuhi, na kuanza mazoezi ya kukimbia, siku zote alipenda kukimbia huku akiimba, kwani alikatiza mitaa karibu yote ya nchi ndogo ya Mwamutapa, bila kujitambua kwani nyimbo alizoimba zilimtia moyo na kumuondolea uchovu. “Ngoja nikimbie, nikimaliza nije kunyenyua vyuma, ukombozi sio lelemama lazima wachache tuumie “,Njoshi aliongea kwa ujasiri huku akitamani siku moja aweze kuishika nchi na yeye kuwa mfalme, huku Grace akiwa malikia, kwani msichana mrembo Grace alipendwa sana na wananchi na aliwaokoa mala nyingi walipokuwa wakionewa na baba yake pamoja na kaka zake, kwani aliwaombea msamaha na kusikilizwa. Walimuona kama ndio kondoo pekee aliyeishi ndani ya kundi la simba. Njoshi alizidi kukimbia lakini bila kutegemea alijikuta akiishiwa na pumzi haraka sana tofauti na siku zingine, bila kupoteza muda aliamua kurudi nyumbani kufanya mazoezi mengine. “Mwanangu kweli wewe ni shujaa, natamani ndoto zako zitimie nikiwa hai nishuhudie ukiwakomboa Wanamutapa wote “,ilikua tayali imeshafika saa moja asubuhi, mama yake Njoshi aliweza kuamka na kumkuta mwanae akiendelea na mazoezi, na kuzungumza maneno makali yaliyomshitua sana Njoshi, haikuwa kawaida kwa mama yake kumwambia maneno mazito kiasi kile. Njoshi alisitisha
mazoezi na kisha kutaka kumuulza mama yake, kwanini alizungumza vile, kwanini mama yake asishuhudie ukombozi ambao mwanae alikuwa akiupanga, mama yake kaona nini mbeleni katabili nini. Njoshi alizidi kujiuliza maswali kichwani mwake, huku akimsogelea mama yake, mke wa marehemu Nyangoma, mganga na mtabili aliyekuwa akitegemewa sana na mfalme Mutapa. Kutokana na kutabili kuwa ipo siku mfalme atamuua kikatili bila kujali mema yote aliyomfanyia, aliamua kumfundisha uganga na utabili mke wake, ili siku akifa mke wake aweze kurithi mikoba. “Mwanangu Njoshi
Nyangoma, naona hatari kubwa iko mbele yako, utasafiri safari ndefu yenye visa na mikasa ya ajabu ,mkanda huu mweusi na panga hili ndio siraha yako kuu, iliyomuwezesha baba yako kutoka salama katika msitu wa majini, usikatae kwenda huko, huko ndipo utaupata ufalme wa nchi hii, lakini ukirudi nyumbani utakuta kabuli langu, mimi nikiwa tayali nimeshakuwa mifupa “,mama Njoshi alizungumza kwa uchungu sana huku machozi yakimtoka, na kumkabidhi mwanae begi dogo jeusi,kwani ndio ulikuwa mwisho wa kuonana yeye na mwanae mpendwa Njoshi. “Sikuelewi mama
unaongea nini, mimi msituni huko niende kufanya nini sasa, kwanza huwezi kufa mimi nitakulinda mpaka dakika ya mwisho “,Njoshi aliongea huku akimfuta mama yake machozi, huku mama yake akiukumbuka ule msemo wa wahenga, msemo ambao ulikua maarufu sana enzi zile afrika ikitawaliwa na wazungu, msemo uliosema jambo usilo lijua ni kama usiku wa giza. Njoshi akiwa
amemkumbatia mama yake, akizidi kumbembeleza aweze kunyamanza, alishangaa kuona kundi kubwa la vijana shupavu, likiwa limevalia bukta fupi nyeusi, pamoja na ngozi ya chui, huku mikononi wakiwa wameshika mikuki na kila aina ya siraha za kivita, bila shaka aliweza kuwatambua, lilikuwa ni jeshi la mfalme Mutapa. “Aiweeeeeeh
………Njoshi, aiweeeeh ………”,askari wale waliweza kumsalimu Njoshi, na kumfanya mama yake kuacha kumkumbatia mwanae na kushuhudia watu wale waliomsalimia mwanae. “Aiweeeeeh ………askari waaminifu wa mfalme wangu wa ardhi ya Mwamutapa, niwasaidie nini? “,Njoshi aliitikia salamu kwa upole na hekima, huku akiificha hasira yake na kisasi kizito kilicho rohoni mwake, kutokana na baba yake kuuawa kikatili na mfalme. Kwa upande wa mama yake
hakushangaa chochote, kwani alikwishaona kila kitu kitakachotokea mbele, na pia siri ya mfalme ambayo wananchi hawakutakiwa kuifahamu, kuhusu kuzikwa mala atakapokufa na kisha kufufuka bila wananchi kutambua chochote, ili aweze kuishi na kutawala milele. “Tumekuletea
ujumbe huu wa maandishi kutoka kwa mfalme, mkwe wako tafadhali pokea ……iweeeeh “askari wale waliongea huku, mmoja aliyeonekana kuwa na cheo kikubwa kuwazidi wenzake kutokana na kuvaa ngozi ya simba, ngozi iliyokuwa ikivaliwa na kila kiongozi wa nchi ya Mwamutapa, akimkabidhi Njoshi karatasi yenye maandishi na kisha kuisoma. “Iweeeeeh …mkwe
wangu, nakuomba katika ikulu yangu, ninashida na wewe, nataka tuwekeane mkataba ili uweze kumuoa binti yangu Grace “,Njoshi alisoma maneno yale na kisha kutabasamu, tabasamu ambalo liliwafanya askari wale wa mfalme kuangaliana na kisha kukonyezana, hali iliyoonesha kutambua siri fulani iliyokuwa imefichika. “Mama peleka begi
“Hapana mwanangu,hili ndani, mimi ngoja nikaonane na mfalme “,Njoshi aliongea huku akionekana kufurahia sana, kwani hakuamini kama ipo siku mfalme atamtamkia kuwa yeye ni mkwe wake,kwani siku zote aliambulia matusi na kutishiwa kifo, alipoingia anga za mfalme Mutapa. kama unanipenda, naomba hilo begi lisitoke mgongoni mwako “,mama yake Njoshi aliongea huku akiwa na huzuni moyoni, huku akijaribu kutabasamu kuficha huzuni yake, kwani huo ndio ulikuwa ni mwisho wa kuonana na mwanae katika ulimwengu huu. |