MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 03*

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SIMULIZI: “JENEZA LA AJABU ” **SEHEMU YA 03*
#1
SIMULIZI: “JENEZA
LA AJABU “
**SEHEMU YA 03*
Msitu wa Majini;
        Ilikua mida ya jioni siku ya jumatatu ,
tetemeko la kutisha linatokea katika msitu wa majini,Malikia wa msituni,
kiongozi aliyemiliki msitu na kuongoza viumbe vyote vilivyopatikana ndani ya
msitu anaamua kuitisha kikao, kwani tetemeko lile liliashiria jambo fulani,
kama ilivyozoeleka katika msitu huo, tetemeko likitokea basi muda wowote msitu
ulikua hatarini kuvamiwa.
“Ndugu zangu
majini, mapepo na mizimu ya mababu zetu, msitu wetu uko hatarini kuvamiwa ,na
niwajibu wetu kuulinda msitu huu, pia inatakiwa tulipize kisasi kwani mtu
anayekuja kuvamia msitu huu, baba yake aliwahi kuja hapa msituni na kuua ndugu
zetu na kisha kutokomea na baadhi ya mali zetu ili awe mganga na mtabili
hodari, japo ameshapoteza maisha “,malikia alizungumza kwa hasira, katika
kikao cha ghafla alichokiitisha muda mfupi baada ya tetemeko kutokea, huku
umati wa viumbe hatari sana wa msitu wa majini, msitu uliokua na utajiri
mwingi, zikiwemo dhahabu na almasi, wakiwa makini kumsikiliza malikia wao na
kujiandaa na mapambano.
“Aiweeee mtukufu
malikia wa msitu huu,tuko tayali kutekeleza maagizo yako, na kuua chochote
kitakachokanyaga ardhi hii “,ilikua ni sauti ya majini waliohudhuria
kikao, huku wakijawa na uchu wa kulipiza kisasi hasa wakikumbuka jinsi mzee
Nyangoma, baba yake Njoshi jinsi alivyofanikiwa kuiba mkanda pamoja na panga
lenye nguvu za ajabu, na kutoroka navyo huku akiua baadhi ya majini, kitendo
kilichowakasilisha viumbe wote wa msituni.
Ikulu kwa mfalme;
Kijana Njoshi anafika ikulu kwa mfalme
na kushangazwa na jambo aliloliona mbele ya macho yake, hali ya mfalme ilikua
mbaya sana kiasi kwamba hakuweza hata kuinuka kitandani wala kufungua kinywa
chake na kutamka neno lolote lile, kwa upande mwingine alitamani mfalme apoteze
maisha kwani aliona ndio utakuwa mwanzo wa ardhi ya Mwamutapa kuwa huru kutoka
katika uongozi wake wa kidikteta ,na pia yatakua ndio malipo ya dhambi zote za
mauaji aliyoyafanya, huku baba yake akiwa miongoni mwa watu waliouawa kikatili
na mfalme.
Njoshi akiwa bado
amepigwa na butwaa, alianza kupata picha kuwa inawezekana aliweza kudanganywa
kuwa aliitwa na mfalme ili aozeshwe Grace,kwani kwa wakati ule, machozi ya
huzuni hayakukatika machoni kwa Grace,na kumfanya aamini mawazo yake, kuwa
palikuwa na tatizo nyumbani kwa mfalme.
“Aiweeeeeh mtukufu
mfalme, mtumwa wako Njoshi Nyangoma nimeitika wito wako, aiweeeeh ……mfalme
Mutapa udumu milele”,Njoshi aliongea huku akiwa amesimama mbele ya kitanda
cha mfalme, huku familia nzima ikiwa imekaa kimya, wakimuomba Mungu Njoshi
akubaliane na ombi la mfalme, kwani waliamini mfalme hata akipoteza maisha
ataweza kufufuka ndani ya wiki moja, jambo ambalo lingewezekana kama angezikwa
ndani ya jeneza la ajabu, jeneza ambalo Njoshi inatakiwa akalitengeneze kwa
kutumia miti inayopatikana katikati ya msitu wa majini na kisha kuja nalo ikulu
kwa mfalme.
“Kijana wangu
Njoshi, utafanikiwa kumuoa binti yangu Grace, na kumiliki nusu ya ufalme wangu,
kama tu ukikubali kwenda katika msitu wa majini, na kutengeneza jeneza kisha
kuja nalo hapa “,yalikuwa ni maneno yaliyoandikwa kwa maandishi na mfalme,
maneno ambayo Njoshi aliyasoma na kisha hofu ya kifo kumuandama, kwani hakuna
mtu aliyewahi kupona kutoka katika msitu wa majini, isipokuwa baba yake
pekee.Njoshi alikumbuka maneno ya mama yake alimwambia kuhusu hatari hii, na
kisha kumsihi asikatae kwenda kwani huko msituni ndiyo sehemu pekee ya kuupata
ufalme, pia Njoshi alikumbuka siraha alizopewa na mama yake na kuziweka ndani
ya begi kisha kumsihi asiweze kulitupa begi hilo.
“Ndiyo mfalme
wangu mtukufu, nimekubali, aiweeeh mfalme udumu milele, “Njoshi alikubali
ombi la mfalme, na kufanya nyuso za familia nzima ya mfalme kutabasamu kwa
furaha, isipokuwa Grace, kwani hakutaka mpenzi wake kwenda msituni ndio maana
alikuwa akilia toka mwanzoni, na wala hakulizwa na hali mbaya ya baba yake
aliyonayo, bali jambo ambalo Njoshi aliweza kuitiwa ikulu, lilikuwa la hatari
sana na aliamini atampoteza mpenzi wake kama atakubali ombi la baba yake.
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 2 Guest(s)